Na Stephen Noel,Timesmajiraonline, Mpwapwa.
WANANCHI wa Kata ya Ghambi wilaya ya Mpwapwa mkoa wa Dodoma wameipongeza na kuishukuru serikali Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Kufuatia mradi wa kumihili mabadiliko ya tabia ya Nchi Kwa kutumia mifumo ya ikolojioa vijijini (EBARR)kuonyesha mafanikio ya kukabiliana na matokeo ya mabadiliko ya tabia ya Nchi ,Kwa kuboresha Huduma za Jamii,zinazoendana na kujikwamua kiuchumi .
Amesema kabla ya mradi huo ilikuwa inawalazima kwenda kata jirani kama za nchunyu au wilaya ya Kongwa ambapo baadhi ya wafugaji walikuwa wanashidwa kutokana na umbali na hivyo kusababisha mifugo mingi kufa.
Wakiongea na wandishi wa habari Kijiji hapo mmoja wa wakazi Kijiji cha Nghambi, Ashery Mogho amesema mradi huo umeweza kuwanufaisha Katika sekta ya mifugo Kwa kupunguza vifo vya mifugo vilivyo kuwa vinatokana na magonjwa ya kung’atwa na wadudu kama kupe na Mbungo.
Solome Sailowa ni mmoja wa wanufaika mradi wa Ebber amesema Kijiji cha Kiegea ni Moja ya Kijiji kilichokuwa kinakabiliwa na Changamoto ya upatikanaji wa Maji safi na salama baada ya mradi huo kuwachimbia kisima kirefu wameweza kuboresha maisha na kuongeza upatikanaji wa mboga mboga kijijin hapo.
Kwa upande wake Diwani wa Kata hiyo bwana Richard Milimo amesema kutokana na mradi wa EBARR( Ecosystem based Adaption for Rural Resilience)umeweza kusaidia kuboresha Huduma za Jamii na kiuchumi Katika kata hiyo kama kuchimba visima vyaMaji, kujenga Majosho ya kuogeshea Ngo’ombe na ,miradi ya vitalu Nyumba, pamoja na miradi kuzuia mmomonyoko wa ardhi ambayo inatekelezwa Katika vijiji vinne vya Ngambi ambavyo ni NG’AMBI,Kazania,Kiegea na Mbugani.
Afisa Kilimo, ushirika na umwagiliaji Wilaya ya Mpwapwa Bi, Mery Lesharu amesema mradi huo Katika wilaya ya Mpwapwa ulijikita Katika kuongeza uwezo wa kuhimili mabadiliko ya Tabia ya Nchi Katika jamii za vijijini Kwa kuimarisha mifumo ya ikolojioa na shughuli mbadala za kuongeza kipato Kwa Jamii za watu Ng’ambi
Mratibu wa mradi wa EBARR wilaya Mpwapwa bwana Azizi Biilu amesema mradi huo tangu kuanzishwa mwaka 2019 wameweza kuwajengea uwezo Wananchi wa kata hiyo kwa juu kuhimili mabadiliko ya Tabia Nchi Kwa kutumia mifumo ya ikolojioa vijijini .
Amesema mradi huo unatekelezwa na Ofisi ya Makamu wa RAIS Muungano na Mazingira ambao umefadhiriwa na mfuko wa mazingira Duniani.
More Stories
TRA kuongeza idadi ya waendesha uchumi walioidhinishwa
TRA Tanga wajivunia ukusanyaji mapato
Wambura asikitishwa na makundi CCM Nyakato