December 28, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Eagle Entertainment kutoa tuzo kwa makundi mbalimbali

Judith Ferdinand, Timesmajira Online, Mwanza

Kampuni ya Eagle Entertainment inayo jishughulusha na masuala ya burudani inatarajia kutoa tuzo kwa makundi mbalimbali mkoani Mwanza ikiwemo waandishi wa habari,wasanii na wajasiriamali Desemba 25,2023 siku ya sikukuu ya Krismasi(Christmas).

Tuzo hizo zitatolewa katika ukumbi wa Mayengera wilayani Sengerema mkoani Mwanza ikiwa ni mwaka wa tatu mfululizo tangu kuanzishwa kwake huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Sengerema.

Akizungumza na Timesmajira Online Mkurugenzi Mtendaji wa Eagle Entertainment Hassan kuku ameeleza kuwa kampuni hiyo imekuwa ikitoa tuzo hizo kwa kada mbalimbali baada ya kutambua michango yao katika jamii.

Kuku ameeleza kuwa kwa msimu huu wa tatu wamepanua wigo kwa kuongeza nafasi za washiriki kutoka Mkoa mzima wa Mwanza tofauti na awali ilikuwa ni kutoka ndani ya Wilaya ya Sengerema.

Hata hivyo ametaja baadhi ya tuzo zitakazotolewa ni pamoja na Mwandishi wa Habari bora wa habari za Mazingira kwa mwaka wa 2023,Msanii Bora wa Kike kwa mwaka 2023,mpiga picha bora wa mwaka,Msanii Bora wa kiume wa mwaka.