December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mwanamfalme Charles wa Uingereza akiwachunga nguruwe wake katika shamba la malisho Guiting Power lililopo Gloucestershire, Cheltenham, Uingereza. Ni baada ya juzi kufanya ziara ya kukagua mifugo yake mjini humo. (Picha na AP).

Duniani katika picha

Baadhi ya watoto kutoka Kijiji cha Mayong wilayani Morigaon Kaskazini Mashariki mwa Assam, India wakiendeshesha mtumbi waliobuni ili kuwavusha katika maji ya mafuriko yaliyokizingira kijiji kutokana na mvua kubwa zilizonyesha juzi huku ikiharibu mali na miundombinu. (Picha na REUTERS).
Mfanyakazi katika moja ya mashamba ya chai wilayani Biswanath Chariali iliyopo Mashariki mwa Jimbo la Assam nchini India akivuna chai kama alivyokutwa juzi. (Picha na AP).
Kondoo wenye alama maalum wakiwa tayari katika eneo la mnada kwa ajili ya kuuzwa mjini Fatehpur, India Juni 27, mwaka huu. (Picha na AP).
Mwanafunzi wa elimu ya juu mjini Lycee Blaise Diagne, Dakar Senegal akinyunyiziwa dawa maalum miguuni kwa ajili ya kudhibiti virusi vya corona (COVID-19) ikiwa ni siku ya kwanza kuwasili shuleni. (Picha na AFP).