Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online
KINARA wa mabao ndani ya klabu ya Azam FC, Prince Dube ataondoka hapa nchini Novemba 29 kuelekea Afrika kusini kwa ajili ya matibabu baada ya kuvunjika mfupa wa mbele wa mkono wake wa kushoto unaoitwa Ulnar.
Mshambuliaji huyo aliumia dakika ya 15 ya mchezo wao wa juzi dhidi ya Yanga ambao walikubali kichapo cha goli 1-0 katika uwanja wao wa nyumbani wa Azam Complex na kushushwa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL).
Taarifa iliyotolewa leo na klabu ya Azam imeweka wazi kuwa, mchezaji huyo anakwenda Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu zaidi baada ya kuvunjika mfupa huo wa mkono Ulnar ambao unaanzia kwenye kiwiko na kushuka hadi kwenye kidole cha mwisho.
“Dube ataondoka nchini Novemba 29 kwa ndege ya Shirika la Kenya Airways (KQ) na atatibiwa kwenye Hospitali ya Vincent Pallotti iliyopo Cape Town, chini ya daktari bingwa wa mifupa, Robert Nicolas,” ilisema taarifa hizo.
More Stories
Naibu Waziri wa Fedha abariki ujio mpya wa Bahati Nasibu
Zanzibar kuzalisha wachezaji wenye vipaji
Othman awakabidhi jezi Zanzibar Heroes