April 15, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Doyo mgombea Urais kupitia NLD

Na Bakari Lulela, Timesmajira Online,Dar

KATIBU MKUU wa chama cha National League for Democry (NLD) Doyo Hassani Doyo amechaguliwa kugombea nafasi ya Urais kupitia chama chake kwa upande wa Tanzania Bara.

Uamuzi huo umetolewa jijini Dar -es-Salaam na kamati kupitia mkutano mkuu wa chama hicho,ambao mbali na Doyo ulimchagua Mfaume Khamisi Hassani kugombea kiti hicho kwa upande wa Zanzibar.

Doyo amesema,maamuzi ya kugombea uongozi wa juu wa nchi ni kutaka kuwaletea maendeleo wananchi kupitia vipaumbele vyake.

“Nimebeba dhima kubwa kwa wananchi wa Tanzania, kuhakikisha nasimamia vyema vipaumbele vyangu ikiwemo ajira kwa vijana, kilimo chenye manufaa ikiwemo pembejeo na masoko, elimu bora kwa makundi ya mbalimbali ya wananchi,”amesema Doyo.

Aidha ameahidi kuleta mapinduzi kwenye sekta ya uchimbaji wa madini kwa kutumia nyenzo bora za kisasa kwa maslahi mapana ya taifa, na kuendeleza uvuvi safi kwa kutumia vyombo vyenye uwezo wa kuvua maji yenye kina.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama hicho, Mfaume Khamisi Hassani,ambaye anagombea kiti hicho kwa upande wa Zanzibar amesema kuwa analinda na kuondoa changamoto mbalimbali zinazowapata wakaazi wa Zanzibar.

Pia ameahidi kudumisha pande mbili za muungano wa Tanzania na Zanzibar kwa kuweka mazingira salama ya kikodi, makazi ili kufanya Zanzibar inakuwa kisiwa cha amani na salama kwa raia wake.

Nae Naibu Msajili wa vyama vya siasa nchini,Six Nyahoza, amevitaka vyama hivyo kudumisha umoja ,amani na kusema siasa sio uadui wala vita hivyo upendo ni silaha katika kuleta maendeleo miongoni mwa watanz