Na Bakari Lulela, TimesMajira Online
KATIBU Mkuu wa National League for Democracy (NLD), Mhe. Doyo Hassan Doyo, pamoja na Naibu Katibu Mkuu Bara, Mhe. Khamis Said Hamad, wakiwa sambamba na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Mhe. Ahmed Salim Hamad, wamekutana na watendaji wote wa makao makuu ya chama katika ofisi za NLD zilizopo Tandika, Temeke, jijini Dar es Salaam.
Katika kikao hicho, pia viongozi hao wakuu walikutana na viongozi wa mkoa wa Dar es Salaam, wakiwemo wenyeviti na makatibu wa wilaya hizo. Viongozi wote walipokea maelekezo muhimu kutoka kwa Katibu Mkuu, Mhe. Doyo, kuhusu maandalizi na mikakati ya kujipanga kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa katika wilaya zao.
Katibu Mkuu Mhe. Doyo aliwataka viongozi hao wa wilaya kuwasilisha majina ya wagombea wenye sifa katika mitaa yao ndani ya muda uliopangwa. Pia aliwataka viongozi hao wawasilishe mipango ya chama katika wilaya zao ndani wiki mbili
“Chama kitaweka wagombea kila mtaa, nendeni mkatuletee wagombea wenye sifa katika maeneo yenu. Tunahitaji baada ya wiki mbili mtuletee mikakati yenu ya uchaguzi,”ameisema Mhe. Doyo.
More Stories
Serikali kupeleka mawasiliano maeneo ya mipakaniÂ
Sekondari ya Butata mbioni kufunguliwa Musoma Vijijini
TIC yapongeza mradi wa Kampuni ya Big Best