DORTMUND, Ujerumani
KLABU ya Borussia Dortmund,imeitolea nje Chelsea ambayo inawania kwa udi na uvumba saini ya mshambuliaji wa timu hiyo, Erling Haaland ili iweze kuimarisha kikosi chao msimu ujao.
Mtendaji mkuu wa Dortmund Michael Zorc amesema bado klabu hiyo ina mipango na Haaland, hivyo msimu huu wa joto mchezaji huyo hauzwi.
Haaland, mwenye umri wa miaka 20 raia wa Norway mshambuliaji anayewania na klabu mbalimbali kwa sasa ulimwenguni ikiwemo Chelsea, Man City pamoja na Real Madrid kutokana na kuonesha kiwango cha hali ya juu.
“Halaand kwa sasa anajiweka sawa nyumbani nchini Norway. Ataungana nasi
huko Dortmund kwa ajili ya mazoezi kesho, hivyo hakuna kilichobadilika bado yupoyupo sana kwetu amesema Mkuu wa Dortmund
Zorc.
Hata hivyo, klabu hiyo bado ipo katika mipango ya kumuongezea mkataba mpya Haaland jambo ambalo litakuwa pigo
kwa Chelsea, ambaye mmiliki wake Roman
Abramovich anahusika na umuhimu wa kutua kwa supastaa huyo katika klabu yake.
More Stories
Zanzibar kuzalisha wachezaji wenye vipaji
Othman awakabidhi jezi Zanzibar Heroes
Rais Samia: Yanga endeleeni kuipeperusha bendera ya Tanzania