JESHI la polisi mkoani Mbeya limesema kuwa kuelekea sikukuu Krismasi na mwaka mpya limejipanga kufanya doria kwa kushirikiana na wananchi kupata taarifa za wahalifu katika maeneo yote ya makanisa ambako watu watakuwa wanafanya ibada.
Kamanda wa polisi Mkoani Mbeya , Benjamini Kuzaga amesema hayo leo kwenye viwanja vya mazoezi vya FFU mkoani hapa wakati akipokea vifaa vya michezo kutoka kwa Spika wa Bunge na Mbunge wa mbeya mjini Dkt. Tulia Ackson lengo likiwa ni kuwahamasisha ushiriki wa michezo kwa jeshi la polisi.
Kamanda Kuzaga amesema kuwa wameshaanza kujipanga ambapo kila kata kuna polisi kata na kuwa polisi kata ana majukumu 17 mojawapo ni kuhakikisha usalama wa eneo hilo akishirikiana na ofisa mtendaji wa kijiji na kata pamoja na wadau .
“Tutahakikisha tunafanya doria maeneo yote ya makanisa na tunachohitaji ni kupata ushirikiano kutoka kwa wananchi ili tuweze kufikia kwa haraka wahalifu ambao ni wabaya katika jamii ili tuweze kuwaondoa sababu wale ni wakataa pema sasa wakataa pema sisi tunajua wapi pa kuwapeleka hatutaki wawasumbue watu wema kwenye jamii “amesema Kamanda Kuzaga.
Aidha Kamanda Kuzaga amesema wamejipanga kuhakikisha kwamba kuna kuna askari wetu wa Intrejesia wapo kukusanya taarifa kutoka kwa wananchi na watendaji na taarifa zitafanyiwa kazi.
“Tumeweka mazingira rafiki ambayo hayatawafanya wananchi kuingia na woga kwa kuona askari kwanza sasahivi wananchi wameanza kuzoea askari ni wachache sana ambao bado wana woga lakini sasa tumepeleka askari kata ambaye ameanza kusogeza jamii karibu na polisi kwa hiyo tumeweka mazingira rafiki kwa wananchi hatuhitaji kumsumbua mwananchi “amesema Kamanda huyo.
Kwa upande wake Spika wa bunge na Mbunge wa Mbeya Mjini , Dkt. Tulia Ackson amelipongeza jeshi la polisi kwa jinsi wanavyofanya mazoezi kwa ajili kukabiliana na mambo yeyote ambayo yanaweza kujitokeza kwenye jamii na kufanya mkoa kutulia na kuwa salama.
“Ni dhahili katika jamii changamoto haziwezi kuisha kwasababu sisi ni binadamu leo tuko hivi kesho tupo hivi kwa hiyo kunakuwa na migongano mara zote lakini mmejitahidi mara zote kuondoa uharifu makosa yanayotokea kwa mmoja mmoja hayawezi kuzuilika niwapongeze sana kwa kazi kubwa hii mnayofanya”amesema Dkt. Tulia.
Akielezea ufanyaji kazi wa jeshi la polisi Dkt. Tulia alisema kuwa katika shughuli zote zinazofanyika polisi wamekuwa msaada mkubwa katika kuweka usalama kwa wananchi .
“Kwenye eneo la michezo huwa tunajitahidi na lina umuhimu wake lakini tunaweza kwenda ngazi nyingine katika kujiweka tayari kwa kufanya mashindano kwa wilaya zote na mimi nitakuwa tayari kuleta zawadi “amesema
More Stories
Wakuu wa Wilaya,Wakurugenzi watakiwa kusimamia programu za chakula shuleni
Mbowe akuna wengi kuhusu maridhiano
Waziri Chana amuapisha Kamishna uhifadhi NCAA, ampa maagizo mazito