December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Dogo Janja atoa msaada kwa wakazi wa Ngarenaro

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online

MSANII wa muziki wa Bongo fleva, Abdulaziz Chende

maarufu kama’Dogo Janja’ametoa msaada wa vitu

mbalimbali kwa wakazi wa Ngarenaro mkoani Arusha kwa

ajili ya kurudisha fadhila katika kitongoji

alicholelewa.

Akizungumzia hilo kupitia kwenye Uurasa wake wa

Instagram Dogo Janja amesema, ameweza kusaidia mahitaj

muhimu kwa familia 40 zisiojiweza.

”Nimepata bahati ya kutembelea mtaa wangu niliozaliwa

nikiwa na timu kubwa ikiongozwa na Djhazuu,tuliweza

kusaidia mahitaji ya muhimu kwa familia (40)

zijisojiweza (Walemavu, Wajane, Wazee, na Watoto).

Licha ya hiyo nimeweza kusikiliza wengine ambao

hawakuwa na uhitaji wa vyakula, bali wao wemekumbwa na

maradhi makubwa sana.

“Na mimi nimeahidi nitashirikiana nao na kusaidiana

nao hadi afya zao zirejee vizuri (Insha’Allah) warudi

kwenye majukumu yao ya kuendelea kulijenga Taifa,”

amesema Dogo Janja.