Na Bakari Lulela, Timesmajira Online,Dar
Chuo cha Bahari Dar-es-Salaam (DMI) na shirika la kimataifa la masuala ya Bahari la Muungano wa Comoro(ANAM),wameingia makubaliano kwa kusaini hati ya ushirikiano.Wenye lengo la kujenga umoja wa utendaji kazi na weledi, katika usimamizi wa vyombo vya maji.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar-es-Salaam Septemba 3,2024,mara baada ya kusaini hati ya makubaliano, Mkuu wa Chuo cha Bahari Dar-es- Salaam,Dkt.Tumaini Gurumo amesema huu ni mwendelezo wa uhusiano ulioanza muda mrefu kati ya Tanzania na Comoro.Ambapo ushirikiano huo umeleta ufanisi, kwani chuo hicho kinafuata taratibu mbalimbali zinazokubalika kimataifa.
Pia Dkt.Gurumo, ameeleza kuwa uhusiano huo,umekuwa na tija kwani yameimarisha ushirikiano kati vijana wa Tanzania na Comoro, na kuhakikisha sekta ya meli inafanya kazi vizuri ili kuinua uchumi na kuleta maendeleo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Kimataifa la masuala ya ubaharia la Muungano wa Comoro,Mohamed Salum, amesema ushirikiano huo ni wa muda mrefu.
“Tumekuwa tukifanya biashara kwa asilimia 80 kutoka Tanzania kwa njia ya meli.Tanzania iko mbele kiutendaji na uwezo,wanafunzi wanaosoma masuala ya meli wana nafasi nzuri Comoro na wana fanya kazi kwa weledi na ufanisi,”ameeleza Mohamed na kuongeza:
“Tunawahamasisha waComoro waje kujifunza mambo ya uendeshaji meli Tanzania, kwani watajifunza mambo mengi ikiwemo lugha ya kiingereza,hivyo wataweza kuendesha meli na kufanya kazi nje ya nchi,”.
More Stories
Wizara ya madini yakusanya bil.521 nusu ya kwanza mwaka wa fedha 2024/25
Meya awafunda wenyeviti Serikali za Mitaa
Mgeja aipongeza CCM kwa uteuzi Wagombea Urais