December 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

DMI yajivunia Wataalamu wanaosanifu na kuzikarabati meli

Na Hadija Bagasha, Timesmajira Online,Tanga

CHUO cha Bahari Dar es Salaam kimeshiriki maonesho ya Elimu,Ujuzi na Ubunifu Jijini Tanga huku wakijivunia kutoa wataalamu wenye uwezo wa kusanifu na kuzikarabati meli kupitia Temesa hivyo kuondoa uhaba uliokuwepo awali nchini .

Ofisa kutoka katika chuo hicho Kapteni Mohamed Kauli ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika maoesho hayo kwa lengo la kueleza wanachokifanya ikiwemo ufanisi wa meli,usafirisha majini,utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi baharini,usanifu injini na ujenzi wa meli na ubaharia.

Amesema awali chuo hicho kilikuwa kinazalisha mabaharia wakati kilipoanzishwa ili kukabiliana na ombwe la ukosefu wa ajira kutokana na vijana wengi kumaliza vyuo na kukosa ajira.

Ambapo ameeleza kuwa wahitimu hao wanafaida kubwa mbili wanapohitimu chuo kupata ajira nchini kwenye sekta ya usafirishaji majini na nje ya nchi kwenye meli.

“Kwa kweli tumekuwa tukizalisha idadi kubwa ya mabaharia wanaofanya kazi nje na ndani ya nchi kuna ‘gepu’ kwenye utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi baharini lakini pia ‘gepu’ la upatikanaji wa meli awali zimekuwa zikiagizwa kutoka nje kwa gharama kubwa,”amesema.

Awali mmoja wa wanafunzi wa chuo hicho,Masaka Julias amesema kwamba mafunzo ambayo wanayapata kwenye chuo hicho yamewawezesha kubuni vitu mbalimbali hivyo wanapomaliza kuweza kujiajiri kupitia ujuzi walioupata.

Amesema kwamba kwa sasa kupitia mafunzo hayo yanawasaidia kutengeneza vitu mbalimbali vya ubunifu huku akieleza kubwa wamebuni wazo la kutengeneza mashine ya kutengeneza chilsource na ya kufunga vifuniko kwenye chupa.