December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Dkt.Yonazi aridhishwa na maandalizi kilele cha mdahalo wa Taifa wa mausuala ya UKIMWI

Na Mwandishi Wetu,Timesmajiraonline,Dodoma.

KATIBU Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi ameeleza kuridhishwa na maandalizi ya kuelekea siku ya kilele cha Mdahalo wa Kitaifa juu ya Mwitikio wa UKIMWI Tanzania itakayofanyika leo Septemba 7, 2023 katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.

Dkt.Yonazi amesema hayo wakati alipotembelea katika ukumbi huo kuangalia maendeleo ya maandalizi hayo yalipofikia.

Ambapo amesema ameridhishwa na hatua ya maandalizi hayo huku akitumia fursa hiyo kueleza mikakati ya Serikali katika kuhakikisha mapambano dhidi ya UKIMWI yanaendelea ili kuyafikia malengo ya sifuri tatu ifikapo 2030.

“Hadi sasa maandalizi yamefikia asilimia 95 hivyo nitoe wito kwa wananchi kufuatilia tukio hili ambalo litarushwa katika vyombo mbalimbali vya habari ili kuendelea kupata uelewa kuhusu masuala ya VVU na UKIMWI”,amesema Dkt. Yonazi

Aidha Dkt.Yonazi ametaja kaulimbiu ya Mdahalo huo kuwa ni“Imarisha ubia na ushiriki wa jamii, kwa mwitikio endelevu wa UKIMWI Tanzania,”