December 27, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Dkt.Tulia:Rais Dkt.Samia amewekeza zaidi ya Trion 6.5 kutatua kero ya umeme

Na Esther Macha,Timesmajira Online, Mbeya

SERIKALI inayoongozwa  chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imewekeza zaidi Trion 6.5 ili kuweza kupata umeme wa uhakika kama nchi kutokana na changamoto ya kukatika umeme mara kwa mara  hapa nchini.

Hayo yamesemwa  leo na Rais wa umoja wa mabunge duniani na Spika wa Bunge ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mbeya mjini Dkt Tulia Ackson wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara na wananchi wa kata ya Isyesye alipokuwa akikabidhi msaada wa madaftari  na sare za Shule kwa watoto 37 wanaoishi katika mazingira magumu kwa shule ya Msingi Ilomba.

Dkt.Tulia amesema kuwa kumekuwa na changamoto ya umeme kama Taifa na si mbeya peke yake na wakati mwingine mgao huo umekuwa  mrefu na vitu kuharibika kutokana na kukatika kwa umeme na wakati mwingine umeme unakatika tu.

“Sasa hiyo changamoto Rais Dkt.Samia amewekeza fedha nyingi zaidi ya Trion 6.5 ili tupate umeme wa uhakika kama nchi sasa wapo watu ambao ni wataalamu wa kupiga maneno hivi na tulishawasikia mlisema mmetusikia tena  wakati mnatusikia miaka mitano iliyopita tulikuwa tunaanza mradi wa bwawa la Mwalimu Nyerere mkatusikia mwaka uliofuata “amesema Dkt.Tulia.

Aidha Dkt.Tulia amesema kuwa mpaka leo hii wameshapita asilimia 95 na  leo hii lile Bwawa  maana yake Nini bado sehemu ndogo Sana ambayo umeme ule utawashwa kila mahali na hata sisi Wana Isyesye tutapata umeme na shule hii ya Ilomba itapata umeme huo.

Akielezea zaidi Dkt Tulia amesema kuwa umeme utakaokuja utatoshereza kwa wote na kwamba mwaka 2024 wataanza kuingiza zaidi  ya  megawaiti 100 kwenye gridi ya Taifa hivyo tatizo la umeme linakwenda kuisha hapa nchini na sio maneno ,wala hadithi ni uhakika.

“Ukitaka kujua kuwa ni uhakika ni kwamba pamoja na changamoto za umeme nguzo zinaendelea kuwekwa maana yake nguzo sio zinawekwa ili watu wasiwe na umeme ,zinawekwa nguzo kwasababu umeme mkubwa unakuja wa kutoshereza kila mwananchi ili.kila kila nyumba iwe na umeme wa kutosha na kata za Pembezoni wanalipa shilingi 27,000″amesema.

Mstahiki wa Jiji la Mbeya ,Dour Issah Mohammed amesema Dkt Tulia aungwe mkono na jamii nao kama viongozi watayatekeleza maagizo kwa vitendo ili aweze kuendelea kusaidia wana Mbeya.

Aidha Meya huyo amesema kuwa wataalamu wa halmashauri ya Jiji la Mbeya wamejipanga kufanya kazi kwa kushirikiana na madiwani wa  Jiji hilo katika kuwatumikia wananchi .