November 21, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Dkt.Tulia:Acheni kuwatelekeza wazazi wenu

Na Esther Macha, Timesmajira Online, Mbeya

JAMII imeaswa kuacha tabia ya kuwatelekeza wazazi na badala yake wawatunze ili wapate baraka badala ya kuachiwa laana.

Kauli hiyo imetolewa Novemba 11,2024 na Rais umoja wa mabunge duniani (IPU)na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Mbeya mjini,Dkt.Tulia Ackson wakati akikabidhi nyumba za kuishi kwa Wananchi waliokuwa wakiishi katika mazingira magumu Jijini humo.

Dkt.Tullia amesema kuwa kati ya wananchi waliokabidhiwa nyumba  hizo mmoja wapo ana watoto wengine wamefariki na wengine wapo hai wamewaacha katika mazingira magumu kwasababu kama wangekuwa hawana uwezo wangewahudumia kwa kiasi wawezavyo.

“Lakini kuwaacha wazazi na kuwatelekeza sio sawa sawa na ni dhambi  kwasababu najaribu kuwaza changamoto hizi sababu naona hili sikuwahi kusikia huko kwingine kwasababu huyo mwingine sikuwahi kumjengea nyumba lakini huyu mwingine tulikuwa tumekarabati nyumba yake yule mtu hatukuwahi kujua kama ana mtoto na tena yupo  hapa Mbeya mjini yule Mzee sisi tukaletewa taarifa tukaenda tukakuta mtoto kajaa mle ndani “amesema Dkt.Tulia.

Hata hivyo Dkt.Tulia  amesema kuwa haipendezi kutekeleza wazazi na kusema iweje mzazi awe mbaya wakati amewalea vizuri amekuzaa,amekunyonyesha,amekulea huna ujualo  na kusema wamekuwa watu wazima wanaona wazazi waathiri maisha yao na kuwa hiyo ni Imani ya uchawi au vyovyote vile  wanavyoamini hiyo ni imani potofu na Imani mfu.

Waliokabidhiwa nyumba hizo ambazo zimejengwa na Taasisi yake ya Tulia Trust ni pamoja na Winifrida Kapingu kutoka ya  Kata ya Ilemi, Bibi Tusekile Kazimoto na Bibi Mwaine Lumbalile wakazi wa Kata ya Iyunga.

“Sio jambo jema Kama sisi kuwa sehemu ya  jamii kuendekeza masuala imani za kishirikina hivyo sasa  ndugu zangu  mnaonisikiliza hapa tuwakumbuke wazazi wetu  na kuwatunza ikiwa ni pamoja na kuwapatia mahitaji yote muhimu unaponiona mimi hapa nami ni mzazi,nami natamani nami siku moja nitumie muda wangu watoto wanitunze ,mzazi aliyekulea toka tumboni mpaka kuwa mtu mzima hawezi kukudhulu “amesema Dkt.Tulia.

Winfrida Kapingu mmoja wa wananchi waliokabidhiwa nyumba na Taasisi ya Dkt.Tulia amesema kuwa amezaliwa upya kwani awali alikuwa analala nje kutokana na nyumba aliyokuwa akiishi kuwa mbovu  na kumfanya yeye familia yake kuishi maisha magumu na na ya Mashaka.

Mmoja wa wananchi waliofika  kushuhudia  tukio hilo la kukabidhiwa nyumba wananchi hao ,Sophia Yuda amesema kuwa Dkt.Tulia anachofanya kwa wananchi wanaoishi katika mazingira magumu ni kitendo cha faraja kubwa na kusema kuwa wapo  watu wenye kipato kikubwa lakini kugusa wenye uhitaji ni wachache na katika 100 ,utakuta wawili.

Mpaka Sasa Taasisi ya Tulia Trust  ambayo ipo chini ya mkurugenzi wake Dkt.Tulia Ackson ambaye ni Spika wa Bunge na Rsis Umoja wa Mabunge duniani na Mbunge wa Jimbo la Mbeya mjini
imejenga nyumba 16 za wananchi wanaoishi katika mazingira ikiwemo mkoa wa Ruvuma .