Na Esther Macha,timesmajira,Online,Mbeya
MGOMBEA Ubunge Jimbo la Mbeya kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dkt .Tulia Ackson amesema changamoto zote katika Kata ya Nonde anazifahamu zikiwemo za ukosefu wa madarasa shule ya msingi Nonde ambapo yeye amechangia mifuko 100 ya saruji.
Aidha amesema shule ya Rejico nayo inakabiliwa na changamoto ya madarasa, ambapo ameahidi atashughulikia changamoto hiyo endapo atachaguliwa diwani, mbunge na Rais kutoka CCM.
Kwa upande wa afya, Dkt. Tulia amesema Serikali imeboresha huduma za afya kuanzia vituo vya afya Ruanda,Igawilo,Hospitali ya Mkoa na Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya.
Hata hivyo amesema mpaka sasa Serikali imeweza kutoa mikopo mbalimbali kwa vijana,wanawake na watu wenye ulemavu.
“Mimi ni mbunge wa kujiongeza ambapo nimetoa bodaboda,bajaj na mikopo na sasa baadhi ya vijana wamejiajiri,” amesema Tulia.
Suala la miundo mbinu amesema baadhi ya barabara zimetengenezwa na zitaendelea kutengenezwa na Serikali endapo atachaguliwa.
Suala la umeme na maji, alisema bado lipo kwenye Ilani ya uchaguzi na atashughulikia endapo atachaguliwa.
Mpaka sasa Dkt Tulia amefanya mikutano katika Kata 32 na akiwa amebakiza kata nne ilhali mpaka sasa Madiwani kumi na sita wamepita bila kupingwa.
More Stories
Rais Samia afurahia usimamizi mzuri wa miradi
Rais Samia apongezwa kwa kuboresha huduma kwa wazee
Watu 5,000 kuhudhuria tamasha la utamaduni Songea