Na Esther Macha,TimesMajira Online. Mbeya
MGOMBEA Ubunge Jimbo la Mbeya Mjini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Tulia Akson amesema baadhi ya wagombea wanaoleta ubaguzi wa kijinsia, hawapaswi kuchaguliwa kwani wamefilisika hoja za kuwashawishi wananchi wawachague.
Amesema baadhi ya wagombea, wamekuwa wakisema kuwa hawezi kuongozwa na wanawake na kusema mtu anayemdharau mwanamke, anakuwa amemdharau mama yake mzazi .
Mgombea huyo amesema, wanawake wana uchungu zaidi na mambo ambayo yanawagusa mfano maji, afya, miundombinu na changamoto nyingine zinazohusu wanawake wenyewe.
Dkt. Tulia ameyasema hayo jana wakati wa mkutano wake wa kampeni katika Kata ya Mbalizi Road Jijini Mbeya, ambako alikuwa akimnadi mgombea Udiwani kupitia CCM, Adam Simbaya.
Amesema kwa kuona umuhimu wa kusaidia miundombinu ya shule za msingi na sekondari, alimeweza kusaidia Shule ya Msingi Mapinduzi iliyokuwa ikikabiliwa na changamoto ya msongamano wa wanafunzi madarasani na uzio wa shule na kusababisha utoro.
More Stories
RC Mrindoko:Ufyekaji wa mahindi Tanganyika si maelekezo ya serikali
Walimu S/ Sekondari Ilala wafundwa juu ya maadili ya wanafunzi
Dkt. Samia afungua skuli ya sekondari Misufini, Bumbwini