Na Esther Macha,Timesmajira,Online, Mbeya
SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Mb) Dkt. Tulia
Ackson amekabidhi jumla ya shilingi Mil.100 ambayo ni mitaji kwa
wanawake 1000 wa mkoa wa mbeya ili waweze kufanya shughuli mbali
mbali za kiuchumi .
Dkt.Tulia alikabidhi mitaji hiyo jana kwa wanawake wa wilaya zote za
mkoa wa Mbeya ambazo ni Wilaya ya Mbeya ,Mbeya mjini , Chunya , Rungwe
, Busokelo ,Kyela , pamoja na Mbarali .
Hata hivyo Dkt. Tulia amesema kuwa wakati mwingne wanawake wanakuwa
na mitaji midogo na kujiunga kwenye vikundi wanakuwa hawana sifa
,Tulia trust inapowawezesha ni kwamba wafanye bidii katika mitaji
waliyopewa msifike mahali nanyi muweze kukopesheka na halmashauri
zenu mikopo inayotolewa na halmashauri zote haina riba .
‘’Na mimi naamini kuwa hakuna mjasiliamali aliyefuatwa nyumbani wote
mmefuatwa kwenye maeneo yenu ya kazi na tunaamini mtaendelea kufanya
kazi hiyo hiyo mliokuwa mkifanya na kuifanya kuwa bora bzaidi na
kukua na kuweza kukopesheka kwenye ngazi ya halmashauri zenu kipekee
kabisa halmashauri ya Jiji sababu ya mapato yake yenyewe inaweza
kutoa Bil .2 kwa mwaka kwa mwakka huu wa fedha unaoendelea na mpaka
sasa zimeshatolewa kwa kiasi kikubwa na zinazosubiriwa ni awamu
zingine ‘’amesema Dkt. Tulia.
Aidha Dkt. Tulia aliwaomba wanawake wa mbeya mjini kujidishisha na
mikopo ili awamu zijazo za mikopo ya halmashauri wawepo kwenye zile
asilimia 4,na hata halmashauri zingine na wilaya wakafanye bidii ili
waweze kuingia kwenye utaratibu mzuri ambapo serikali ya awamu ya Nne
inafanya kazi kuwawezesha akina wanawake.
Kwa u;pande wake Mkuu wa wilaya ya Mbeya , Beno Malisa amesema kuwa
tukio hilo ni adimu kwa miaka mitatu mfululizo la kuwawezesha
wanawake kiuchumi.
Mkuu huyo wa Wilaya amesemma kuwa uwezeshaji kiuchumi kwa wanawake ni
jambo la faraja sana ,matukio yote ya kimaendeleo yanaamusha hali ya
kiuchumi kwa wananchi hasa katika hali ya uchumi kwa vijana na
wanawake tuna vijana wengi wakiinuka kiuchumi.
‘’Akina mama mitaji mliyopewa muende mkaitumie vizuri ili muweze
kuinua familia zenu na lengo kusudiwa , hivi sasa Mbeya hatupoi kwa
shughuli ninazoziona hapa jinsi Tulia Trust inavyofanya , kkumekuwa
na wabunge wengi lakini huyu ni mfano hivyo itakuja kuwa ngumu kumpata
Mbunge wa aina ya kama Tulia ,nawaombeni ndugu zangu tumuunge mkono,
tummshike mkono Mbunge wetu na Spika wa Bunge Mbeya iwe ya mfano
katika Majiji’’amesema Dkt.Tulia.
Mwenyekiti wa bodaboda mkoa wa Mbeya , Aliko Fwanda amesema kuwa
vijana wamekuwa wakinuifaka na Taasisi ya Tulia Trust na mpaka sasa
wana bodaboda ambazo wamekopa zaidi ya 200 na mpaka sasa ana vijana
ambao wamekopa bajaji 120 ambao wamehamia kwenye bajaji kutokea kwenye
bodaboda.
‘’Mimi ni mwana CHADEMA mnafahamu vizuri lakini nitaongea ukweli
kwamba kwa muda wa mihemko haipo tena tulikuwa tunachagua viongozi
kwa mihemko na ikatukosti lakini sasa hivi mbeya mjini tunajitambua
na tumekuchagua Dkt. Tulia wewe ndio Mbunge wetu ,’’Mwenyekiti
bodaboda Fwanda .
More Stories
Maghorofa Kariakoo mikononi mwa Tume
ITA chatakiwa kutoa mafunzo ya viwango vya juu na kasi ya maendeleo ya Kisayansi
Wagombea CHADEMA wakipewa ridhaa,watakuwa wawazi