Na Esther Macha,TimesmajiraOnline,Mbeya
SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU),Dkt.Tulia Ackson, kupitia Taasisi yake ya Tulia Trust ameigusa familia ya Lusia Kapangala mkazi wa mtaa wa Mwasote kata ya Itezi jijini Mbeya ambayo ilikuwa imekata tamaa ya maisha kutokana na hali duni ya kukosa mahitaji muhimu ikiwemo chakula, mavazi na fedha za kusomesha watoto.
Dkt.Tulia amesema pamoja na kuihudumia familia hiyo mahitaji muhimu, pia amechukua jukumu la kuwasomesha watoto wote wa familia hiyo, akiwemo kijana Nature Nenelo aliyehitimu kidato cha nne mwaka 2024 na kupata ufaulu wa daraja la kwanza la alama 13 na kushindwa kuanza masomo ya kidato cha tano kutokana na Bibi yake kukosa fedha.

Aidha Dkt.Tulia alishukuru ubalozi wa Lameki kwa jitihada Kubwa za kuhakikisha kuwa wanaisaidia familia hiyo iliyo kwenye mazingira magumu.
“Leo hapa tumekusanywa kwa jambo la kheri wana ubalozi wa Lameki michango waliyotoa kwa familia ili waweze kwenda shule tunawashukuru Sana,sasa kuanzia leo jukumu hili litachukuliwa na Tulia Trust na sio kuwa wenye nacho washindwe kusaidia familia hiyo, Lakini lile jukumu la kiujumla kabisa la mahitaji makubwa yote litachukuliwa na Tulia Trust hivyo hakutakuwa na uratibu tena wa kuhitaji michango tena”amesema Dkt.Tulia.
Aidha amesema pia wamekusanyika kutambua jitihada zake katika elimu na kumpongeza kijana Neture ambapo Taasisi ya Tulia Trust imegharamia zote za mwanafunzi huyo mpaka amalize elimu yake.
“Si kawaida kwa mtoto anayetoka kwenye mazingira magumu akaweza kutia bidii katika masomo,na sababu za kutofanya vizuri anazo kwasababu nyumbani kuna muda kuna njaa, viatu hana, daftari kuloa,lakini yeye amefanya bidii ili asionyeshe sababu kufeli, lazima sisi Jamii yote lazima tumpongeze “amesema Dktr Tulia.
Kwa upande wake, kijana Nenelo ameeleza namna alivyopitia ugumu katika safari yake ya masomo ikiwa ni pamoja na kukata tamaa ya kuendelea na masomo ya kidato cha tano baada ya familia kukosa fedha za kumudu kusomesha watoto wawili, yeye pamoja na kaka yake anayesoma chuo, Huku Bibi yao Bi. Lusia Kapangala akimshukuru Dkt. Tulia pamoja na wananchi kwa kuwa msaada kwao katika kipindi chote.
Kijana Nenelo amesema kuwa amezaliwa Kwenye familia yenye mazingira magumu kwa kuelewa na bibi ambaye hakuwarna uwezo wa kipato.
Amesema alipofaulu alishindwa kuendelea kutokana na hali ya kimaisha waliyonayo kiasi hata chakula kuwa changamoto hata mavazi walikuwa wakitegemea kwa majirani ili waweze kuishi.

More Stories
Bilioni 7 kuwainua vijana 308 sekta ya uvuvi
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako