December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Dkt. Tax akutana kwa mazungumzo na Balozi wa Uingereza

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb) amekutana kwa mazungumzo na Balozi wa Uingereza nchini, Mhe. David Concar katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Pamoja na mambo mengine, viongozi hao wamejadili namna ya kuboresha uhusiano baina ya Uingereza na Tanzania na jinsi ya kufanya kazi kwa pamoja katika kudumisha na kuendeleza uhusiano huo.