June 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Dkt.Sweke aeleza Uvuvi wa Bahari Kuu ulivyoongeza pato la Taifa



Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma.


MAMLAKA ya Kusimamia Uvuvi wa Bahari Kuu imesema kuwa kwa kipindi cha mwaka 2022 hadi kufikia wiki mbili zilizopita uvuvi wa bahari kuu umeingiza pato la taifa kiasi cha sh.bilioni 4.1 kwashughuli za utoaji wa leseni kwa meli za uvuvi.

Hayo yameelezwa jijini hapa leo,Februari 8 ,2023 na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Kusimamia Uvuvi wa Bahari Kuu,Dkt.Emmanuel Sweke alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Maendeleo ya mamlaka hiyo toka imeanzishwa kisheria mwaka 2010.

Dkt.Sweke amesema kuwa pamoja na Uvuvi kuwa ni gharama kubwa lakini umeweza kuliingizia pato taifa kwa njia za utoaji leseni kwa meli za ndani na nje ambazo zinataka kufanya biashara ya uvuvi katika bahari kuu.

Ambapo amesema mwaka 2010 walitoa leseni kwa meli za uvuvi 536 na mwaka 2015 walitoa leseni kwa meli za uvuvi 596.

“Mamlaka ya kusimamia uvuvi wa bahari kuu umekuwa na majukumu mbalimbali ikiwa ni pamoja na utoaji wa leseni kwa meli ambazo zinatakiwa kufanya uvuvi na kuhakikisha zinapokuwa zimepewa leseni zinakuwa na bendera ya Tanzania,

“Pamoja na kuwa na bendera ya Tanzania lazina kuwepo na usimanizi wa kulinda usalama wa wavuvi na meri zao huku kuhakikisha hakuna uvuvi haramu ambao umekuwa ukijitokeza katika bahari hiyo”ameeleza Dkt.Sweke.

Katika hatua nyingine amesema kuwa mamlaka katika kulinda usalama wa bahari kuu wamewekamifumo ya kulinda usalama ikiwa ni pamoja na kutumia mifumo ya kufuatilia meri ndani ya maji na kutumia doria za ndege kwa ajili ya kuangalia kinachofanyika.

Dkt.Sweke amesema kuwa Mamlaka hiyo inatoa leseni kwa ajili ya uvuvi wa samaki aina ya jodani na kueleza kuwa inapotokea mwombaji anafanya tofauti ukamatwa.

Pia Dkt.Sweke amezungumzia maendeleo ya mapato ndani ya bahari kuu ambapo amesema tayari mwekezaji kutoka nchini hispania anatarajia kujenga kiwanda cha kuchakata samaki ambacho kitajengwa katika bandari ya Tanga .

Amesema kuwa mpaka kiwanda hicho kikamilike kitagharimu kiasi cha dola milioni 10,kitazalisha ajira kwa watanzania 100 na kinatarajiwa kuchakata takribani tani 200 kwa siku.

Vilevile ameeleza kuwa bado mamlaka inakabiliwa na changamoto ya ajira ya moja kwa moja hivyo wapo katika mkakato wa kuanza kutao ajira kwa maafisa na waangalizi.

Aidha amesema toka Mamlaka kuanzishwa imefanikiwa kukamata meri moja iliyokuwa na samaki tani 100 ya samaki wasiolengwa.