Na Waandishi Wetu, TimesMajira Online, Dodoma
RAIS wa Zanzibar Dkt Ally Mohamedy Shein amewaomba wanachama wa chama cha Mapinduzi (CCM) na wananchi kwa ujumla Visiwani zanzibar kumchagua Dkt Hussein Mwinyi kuwa Rais wa Zanzibar na Dkt.John Magufuli kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwani wanatosha na wanavigezo vyote vya kuwatumikia wananchi katika nafasi hiyo.
Akizungumza leo katika uzinduzi wa kampeni za chama hicho amesema Dkt Mwinyi ni mzalendo na anapenda maendeleo lakini pia ni mchapakazi hivyo zanzibar itakuwa katika mikono salama.
“Ndugu zangu Mwinyi anatosha sana tena sana kijana huyu ni mchapa kazi na mpenda maendeleo niwaombe mumchague kwa kura nyingi za ndio ili aweze kuiwatumikia wanazanzibar,”alisema Shein.
Pia amewaomba wananchi kumchagua tena Dkt.John Magufuli na Makamu wa Rais mama Samia Suluhu Hassan pamoja na viongozi wengine wa ngazi za chini kupitia chama cha mapinduzi.
“Kumchagua Rais na Makamu pekee haitoshi ni lazima tuhakikishe tunachagua na viongozi wa ngazi za chini ikiwa ni pamoja na Wabunge na Madiwani ili wakafanye kazi nzuri tena kwa ushirikiano,”alisema .
Amesema,yaliyofanywa na Rais Magufuli ni mengi na yanaonekana wala hayajifichi,hivyo hakuna mashaka dhidi ya utendaji wake.
Kwa upande upande wake mgombea urais kupitia CCM Dkt.Hussein Mwinyi ametumia fursa hiyo kuwakumbisha wanachama wa chama hicho kujitokeza Siku ya uchaguzi kwenda kupiga kura licha ya kujihakikishia ushindi.
Vile vile amehimiza kulindwa kwa jamani nanutulivu huku a kuwataka bwana chama hao kutokubali kutumika katika kuvuruga tunu hiyo.
“Kuna viashiria vya uvunjifu wa amani na vimeanza kuonekana na kuzuntumzwa na baadhi ya watu ,nawaombeni msikubali kutumika kuvuruga amani.” Amesema Dkt.Mwinyi Alitoa salama za wanachama wa chama hicho visiwani Zanzibar amesema,wapo tayari kuchagua CCM wanachosubiri ni Siku ya kupiga kura tu.
Amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Magufuli na Rais wa Zanzibar Dkt.She in kwa kazi kubwa waliyoifanya huku akisema tayari wamerahisisha kazi ya uchaguzi.
Baadhi ya wagombea ubunge walipata nafasi ya kuzungumza machache ambapo pamoja na mambo mengine walimwombea kura Dkt.Magufuli
Mgombea ubunge jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde amesema mambo mengi yamefanyika Dodoma na Tanzania kwa ujumla.
“KimsingibRais umefanya mambo katika mkoa wetu wa Dodoma na Tanzania kwa ujumla,kama watu hawatasema haya basi hata mawe yatainuka kuyasema” amesema Mavunde
Naye Mgombea wa Kongwa Job Ndugai amesema kampeni za mwaka huu pamoja na mikutano ya mihadhara kampeni yetu iwe rahisi ya kufikia kaya kwa kaya.
“Umuhimu ni uwezo wa kuamua,wanaccm na wananchi kwa ujumla waamue kuchagua wabunge madiwani na Rais kutoka CCM kwa ajili ya maendeleo zaidi.”
Amesema tayari wameanza maandalizi ya bunge la 12 ambalo litakuwa la kisasa zaidi.
More Stories
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba
27 kulipwa kifuta jasho Nkasi
Mwakilishi Mkazi wa UN nchini awasilisha hati