March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Dkt.Samia :Sasa hivi Dar hakuna tatizo la umeme kukatikakatika na ukikatika kunasababu zinazotolewa

Na Penina Malundo,Timesmajira

Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema kuwa mkoa wa Dar es Salaam kwa sasa hakuna tatizo la Umeme na endapo umeme ukikatika kunakuwa na sababu maalum zinazotolewa.

Akizungumza hayo jana jijini Dar es Salaam katika Mkutano wa Kampeni viwanja vya Leaders wakati akihutubia wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam amesema sio muda mrefu uliopita kulikuwa na kilio cha umeme kukatikakatika,umeme kuwaka kwa zamu ,umeme kutotosheleza lakini kwa sasa umeme upo masaa 24 kwa siku zote saba.

“Kwa sasa hivi umeme ni twenty four seven na ukizimwa kuna matangazo kwanini umezimwa na kuna sababu utolewa kwanini umezimwa ,”amesema Rais Samia