Judith Ferdinand,Timesmajira online, Mwanza
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan anatarajia kuwasili mkoani Mwanza Juni 12,2023 kwa ajili ya uzinduzi wa tamasha la Bulabo pamoja na kutembelea miradi ya kimkakati ilipo mkoani hapa.
Akizungumza katika kikao cha wakuu wa taasisi zinazosimamia miradi ya kimkakati katika mkoani Mwanza kilichofanyika Juni 8 mwaka huu,Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Amos Makala,ameeleza kuwa Rais atawasili mkoani hapa Juni 12, mwaka huu hivyo Juni 13 atazindua tamasha hilo kisha Juni 14 atatembelea miradi ya maendeleo ya kimkakati.
Tamasha hilo litazinduliwa na Rais Samia Juni 13,2023 linalofanyika eneo la Bujora Kata ya Kisesa wilayani Magu mkoani Mwanza sambamba na kukagua maendeleo ya miradi ya kimkakati ikiwemo ujenzi wa daraja la Kigongo Busisi,meli ya Mv.Mwanza hapa kazi tu pamoja na jengo la NSSF hotel.
“Chifu Hangaya anarudi kule alipopewa uchifu,kwaio tutakuwa na tamasha kubwa na maandalizi yanaendelea yapo katika hatua nzuri na Juni 14 katika Mkoa wetu Rais atapita katika miradi mbalimbali ya maendeleo na kufuatilia mradi wa Kigongo-Busisi,meli kubwa na hoteli ya NSSF,”ameeleza Makala.
Hivyo ametumia fursa hiyo kuwaomba wananchi wa Mkoa wa Mwanza kujitokeza kumpokea Rais kwa siku hizo zote hatakazo kuwa mkoani hapa.
Sanjari na hayo Makala amewataka wakuu wa taasisi hizo kuhakikisha wanasimamia na kuzitatua changamoto zinazokabili miradi ya maendeleo ili iweze kukamilika kwa wakati na kuleta tija kwa wananchi.
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa