December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Dkt.Samia kupigiwa kura nafasi ya uenyekiti CCM Taifa

Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma

KAMATI Kamati Kuu ya CCM imemteua Mwenyekiti wa Chama hicho aliyepo Madarakani  ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan  kugombea tena nafasi hiyo kwa kipindi Cha miaka mitano  ijayo lakini pia imemteua  Makamu Mwenyekiti Bara anayemaliza muda wake  Abdulhaman Kinana kugombea nafasi hiyo .

Aidha Kamati Kuu ya Chama hicho imemteua Rais wa Zanzibar Dkt.Hussein Ally Mwinyi  kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti Zanzibar nafasi inayoachwa wazi na Makamu Mwenyekiti Zanzibar Dkt.Ally Mohamed Shein ambaye anamaliza muda wake kutokana na kustaafu.

Akitoa tamko la Halmashauri Kuu ya CCM iliyoketi leo Makao Makuu ya CCM Taifa  Jijini Dodoma ,Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama hicho Taifa  Shaka Hamdu Shaka amesema viongozi hao watachaguliwa kwenye Mkutano Mkuu wa 10 wa chama hicho utakaofanyika Desemba 7 na 8 mwaka katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Convertion ambapo amesema ,mbali na kuwachagua viongozi wa hao ngazi ya juu ya Taifa,pia mkutano huo utawachagua wajumbe wa Halamshauri Kuu ya CCM Taifa kupitia viti 15 bara na viti 15 Zanzibar ambapo jumla ya wananchama wa chama hicho 2,047 wamegombea nafasi hizo .

Kwa upande wa Bara halmashauri Kuu ya CCM imewateua wanachama 251 kuwa wagombea wa nafasi za ujumbe wa halmashauri Kuu ya CCM Taifa ambao pia watapigiwa kura siku ya kesho

Kadhalika kwa upande wa Zanzibar nako Halamshauri Kuuu ya Taifa ya CCM imefanya uteuzi wa wanachama 123 kuwa wagombea kwa nafasi hizo za wajumbe wa Halamshauri Kuu ya Taifa ambao wote wataungana kwenda kupigiwa kura siku ya kesho

Kwa hiyo kazi moja ya Mkutano Mkuu wa Kumi ni kumchagua mwenyekiti wa wa CCM kwa ngazi ya Taifa na Makamu wake wawili lakini pia kuwachagua wajumbe wa halmashauri Kuu ya Taifa kwa nafasi 15 bara na 15 Zanzibar

Kazi nyingine ni kupokea taarifa ya utekelezaji wa kipindi cha miaka mitano ya kazi za CCM kuanzia 2017 hadi 2022 pia kazi nyingine ni kupokea taarifa ya utekelezaji wa ilani ya CCM kutoka serikali zote mbili kwa bara na Zanzibar ambapo kwa bara taarifa itawasilishwa na waziri Mkuu na Zanzibar itawasilishwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar . 

Aidha Shaka amesema, kazi nyingine itakayofanywa na Mkutano huo ni kupokea taarifa ya utekelezaji ya kipindi cha miaka mitano ya kazi za CCM kuanzia 2017 hadi 2022.

Katika hatua nyingine Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imempongeza na  kumtambua Dkt.Shein kwamba uenyekiti wake ulibeba umahiri wa hali ya juu ukizingatia weledi uadilifu,uzalendo busara na hekima kwa nyadhifa zote alizoshika kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Zanzibar na ndani ya CCM .

Chama cha Mapinduzi Desemba 7 na Desemba 8 kinakutana Jijini Dodoma katika Mkutano Mkuu wa 10 kwa ajili ya kujadili mambo mbalimbali lakini kubwa likiwa ni kupitisha jina la Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa,Makamu Mwenyekiti Bara na Zanzibar pamoja na wajumbe 30 wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kupitia viti 15 Bara na Zanzibar viongozi ambao watakitumikia chama katia nyadhifa hizo kwa kipindi cha miaka mitano yaani kuanzia 2022 hadi 2027.