Na Judith Ferdinand, Timesmajira online,Mwanza
Rais Samia Suluhu Hassan, amemuagiza Waziri wa Maji Juma Aweso na watendaji wa Wizara hiyo wa Mkoa wa Mwanza kuhakikisha wanafufua visima vya zamani ili wananchi wapate maji safi na salama.
Dkt Samia ametoa kauli hiyo wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa tamasha la utamaduni Bulabo linalofanyika Kisesa wilayani Magu mkoani hapa.
Amesema ni kweli ameisha toa kiasi cha bilioni 69 kwa ajili ya mradi wa mkubwa wa maji Mwanza wa Butimba na anajua kupata maji ni hatua lazima mambo kadhaa yafanyike na kwa mwanadamu kusubilia maji ni adha kubwa.
“Najua shida kubwa ya maji ipo ndani ya mji huu kwa maana hiyo namuagiza Waziri wa Maji na watendaji wake katika Mkoa huu kuangalia uwezekano wa kufufua visima vya maji wakati watu wanasubilia mradi mkubwa wa maji lakini visima vya zamani vianze kutoa huduma za maji safi na salama kwa wananchi wa Mwanza,”amesema Dkt Samia.
Huku akiwahimiza wananchi kila mmoja kwa nafasi yake kufanya kazi kwa bidii ili kuendeleaza taifa kwani serikali pekee yake haiwezi.
Mmoja wa wananchi wa Kisesa Leocadia Nestory, ameeleza kufurahishwa na agizo hilo la Rais ambapo likitekelezwa kwa wakati litasaidia kuwaondolea adha ya maji ambayo inawasumbua kwa muda mrefu.
More Stories
Watoto wenye uhitaji wapatiwa vifaa vya shule
Wananchi Kisondela waishukuru serikali ujenzi shule ya ufundi ya Amali
RC.Makongoro ataka miradi itekelezwe kwa viwango