Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online
Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ameendelea kuinua hadhi ya Tanzania kimataifa,ambapo ameingizwa katika orodha ya Forbes ya mwaka 2024 ya wanawake 100 wenye nguvu zidi duniani.
Alipoingia madarakani mwaka 2021, Rais Samia ameandika historia kuwaa Rais wa kwanza mwanamke wa nchini Tanzania,tangu wakati huo ameongoza taifa kwa uthabiti, akitetea misingi ya kidemokrasia, kushiriki katika uwezeshaji wa wanawake, na kuongoza mageuzi ya kijamii na kiuchumi.
Falsafa yake ya “4Rs” yani Maridhiano, Ustahimilivu, Mageuzi, na Kujenga Upya,imekuwa msingi wa kuimarisha mshikamano na kukuza maendeleo endelevu.
Kiongozi mwenye maono na ushawishi wa kimataifa
Ushawishi wa Rais Samia unazidi mipaka ya Tanzania,uongozi wake siyo tu umeimarisha utulivu wa nchi baada ya mpito mgumu bali pia umeiweka Tanzania kama mchezaji muhimu katika siasa za kikanda na kimataifa.
Uenyekiti wake wa hivi karibuni wa SADC ni ushahidi wa uwezo wake wa kidiplomasia.
Mtazamo wake wa maendeleo shirikishi, haki za wanawake, na uendelevu wa mazingira unatafsirika kimataifa, ukiendana na malengo makuu ya agenda ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa.
Kuwawezesha Wanawake na Kufafanua Upya Uongozi
Kutambuliwa kwa Samia na Forbes ni tamko lenye nguvu kuhusu nafasi yake ya kufafanua upya uongozi barani Afrika na duniani.
Kama kiongozi mwanamke, anaendelea kuwahamasisha mamilioni ya wanawake na wasichana, akithibitisha kwamba jinsi si kikwazo cha kufikia mafanikio.Serikali anayoiongoza imetoa kipaumbele kwa usawa wa kijinsia, kuhakikisha wanawake wanakuwa na nafasi katika meza ya maamuzi.
Kichocheo cha Ukuaji na Mabadiliko
Chini ya uongozi wake, Tanzania imepiga hatua katika miundombinu, afya, na elimu. Sera zake madhubuti za kiuchumi zimevutia uwekezaji wa kigeni na kuimarisha nafasi ya Tanzania kama nguvu inayochipukia kiuchumi Afrika Mashariki.
Kusherehekea urithi unaotengenezwa
Kutambuliwa kwa Rais Samia Suluhu Hassan na Forbes siyo tu kutambua mafanikio yake binafsi, ni kusherekea uwezo na ustahimilivu wa Tanzania. Anapoongoza taifa kuelekea mustakabali mzuri, sifa zake za kimataifa zinathibitisha nafasi yake miongoni mwa viongozi wenye ushawishi zaidi duniani.
More Stories
Ripoti ya uchumi yaonesha matokeo makubwa Tanzania
Furaha ya kila mwanamke ni kuwa mama
Ijue nyota yako ili kufanikiwa kimaisha, mahusiano na ndoa