January 23, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Daktari – watoto kutoathiriwa na Covid -19

Judith Ferdinand, Mwanza,timesmajira Online

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dkt.Thomas Rutachunzibwa, amesema sababu ya chanjo ya UVIKO-19,kutotolewa kwa watoto wenye umri wa miaka 6-17, ni kutokana na kundi hilo kutoathiriwa na ugonjwa wa corona.

Dkt.Rutachunzibwa,ameyasema hayo hivi karibuni wakati akitoa ufafanuzi wa maswali yalioulizwa na baadhi ya waandishi wa habari mkoani Mwanza,wakati wa mkutano wa maswali na majibu juu ya UVIKO-19,baina ya waandishi wa habari wa Mkoa wa Mwanza na Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.

Amesema,katika afua zote za afya kinacho waongoza ni sayansi,kwa wagonjwa ambao wanawapokea hivi sasa wa corona,kundi la watoto aliathiriki siyo nchini hapa hata nje ya nchi.

Kilichojitokeza sasa hivi watoto hawapati ugonjwa ila virusi vinaingia mwilini,kwa sababu kuna maumbile kwenye mapafu au kwenye chembechembe za mwili,ambayo yanawafanya watoto wasipate ugonjwa huo wa corona.

Hivyo amesema,hawawezi kupeleka rasilimali kwenye sehemu ambayo haitaleta matokeo,sasa kama kundi aliathiriki wanapelekaje chanjo tena,lazima waelekeze kwenye yale makundi makubwa ambayo yapo kwenye hatari kubwa zaidi.

Pia amesema,ukiangalia maumbile ya kile kirusi kina nundu nundu zile ambazo zikiingia mwilini zinaenda kujishikiza kwenye chembe za mwili mule ndani,sasa kwa watoto yale mapokeo ya virusi kwenye zile chembe chembe za mwili hazina zile resepta ambazo vile virusi vikatua.

Hivyo kama virusi havina sehemu ya kutua vitakaa mwilini mpaka vinakufa kwa sababu mpaka kijiingize na kianze kuathiri seli ndio kiishi,kwaio kikikaa mwilini bila kupata risepta kinaangamia chenyewe.

“Kwahiyo kwa watoto zile risepta ni chache,ndio maana watoto hawapati madhara kwa sababu hawana mapokeo ya vile virusi,kwaio kama huo ugonjwa hauwashambulii hamna haja ya kupeleka chanjo kwa sababu hawapo kwenye hatari ya kupata ugonjwa,”amesema Dkt. Rutachunzibwa.

Hata hivyo amesema,mambo yanabadilika inawezekana kirusi kikabadilika kikaja kirusi kipya chenye mabadiliko ambayo yanaweza kuathiri seli lakini kwa virusi vilivyopo sasa,seli za mwili wa mtoto hazina mapokeo ya virusi hivyo.

Sanjari na hayo amesema,katika suala la chanjo ya UVIKO-19 mkoani humo mwako mkubwa wa wananchi kuchanja ni kutoka vijijini hasa katika wilaya za Kwimba,Misungwi na Magu,hivyo aliwaomba waandishi wa habari kuwahimiza wananchi wanaoishi mijini kwenda kuchanja.

Kwa upande wake mmoja wa waandishi wa habari mkoani Mwanza, Elizabeth Faustine,amewaomba timu ya wataalamu wa afya, kuendelea kutoa elimu zaidi kuhusiana na suala zima la chanjo ya UVIKO-19 ikiwemo sababu za makundi fulani kutopatiwa chanjo hiyo na mengine kupatiwa ili kuondoa maswali mengi na mtazamo uliojengeka kwa jamii.