December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mbunge wa Jimbo la Kigamboni Dkt.Faustine Ndugulile akionyesha fomu yake aliyochukua leo akiambatana na Wanachama wa Chama cha CCM waliomsindikiza.

Dkt.Ndungulile achukua fomu rasmi ya kugombea ubunge Kigamboni

Na Penina Malundo,TimesMajira ,Online

ALIYEKUWA Mbunge wa Jimbo la Kigamboni Dkt.Faustine Ndugulile amechukua fomu leo ya kutetea  nafasi yake kwa mara ya tatu ya ubunge.

Hatua hiyo imekuja baada ya  jana kuteuliwa na  Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM TAIFA kumptisha rasmi kuwa mgombea ubunge jimbo la Kigamboni kupitia tiketi ya Chama hicho.

Dkt.Ndugulile amechukua fomu hiyo katika Ofisi ya Mkurugenzi wa wilaya ya Kigamboni leo majira ya mchana.