December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Dkt Nchimbi awataka Watanzania kudumisha amani na Upendo

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online

KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Taifa Balozi Dkt Emanuel Nchinbi, amewataka watanzania kuendelea kudumisha amani na upendo iliyopo nchini, huku akitoa rai kwa Watanzania kumuombea Dua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kutokana na Kufanya kazi kubwa ya Kizalendo ya kuwaletea maendeleo Wananchi.

Katibu Mkuu huyo wa CCM Dkt. Emanuel Nchimbi alisema hayo Katika IFTAR na Dua Maalum iliyoandaliwa na Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa iliyolenga kumuombea Dua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan na kufuturisha yatima .

“Tudumishe amani na upendo katika nchi yetu tumuombee dua zaidi Rais wetu na UVCCM Taifa kwa mapenzi makubwa sana ya nchi yetu kwa kuandaa futari na dua Maalum “alisema Dkt.Nchimbi.

Alipongeza madrasat Annujum Litahfidhi Al Qurani kwa dua nzuri na kuandaa vijana katika misingi ya dini na kuwataka viongozi wote kuipenda nchi yao .

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa Mohamed Kawaida ,alisema dhumuni la kuandaa futari hiyo ni kufuturisha yatima pamoja na Dua maalum kwa ajili ya Dkt Samia Suluhu Hassan.

Mwenyekiti wa UVCCM Taifa alisema katika futari hiyo pia walitoa vyeti vya shukrani kwa taasisi za dini na vikundi vya yatima.

Nae Meya wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam Omary Kumbilamoto alitumia fursa hiyo kuwapongeza Jumuiya ya umoja wa vijana kwa kuandaa jambo hilo kubwa ambapo pia alipongeza taasisi za kiislam kwa dua nzuri kwa ajili ya kumuombea Rais Dkt.Samia .

Meya Kumbilamoto aliomba jumuiya hiyo ya UVCCM Taifa ifanye kazi zake vizuri ili uweze kuongoza jumuiza hiyo ili waweze kufikia malengo yake ikiwemo kuongeza wanachama wengi.