Na Cresensia Kapinga, TimesmajiraOnline,Songea
KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amewaondoa hofu wakulima mkoani Ruvuma akisema Serikali wa pembejeo za kilimo, hivyo zitauzwa kwa bei elekezi ambazo ni rafiki kwa mkulima na si vinginevyo.
Dkt. Nchimbi ameyasema hayo jana wakati alipopokelewa na mamia ya wakazi wa Mkoa wa Ruvuma katika eneo la Mji Mdogo wa Madaba, ambako alisalimia wananchi wakiwemo viongozi wa Serikali.
Amesema Mkoa wa Ruvuma ni miongoni mwa mikoa mitano inayozalisha chakula kwa wingi nchini, hivyo Serikali lazima ione umuhimu wa kupeleka pembejeo kwa wakati ili uzalishaji uweze kuongezeka zaidi na mulima aweze kuongeza uchumi katika familia zao.
Balozi Dkt Nchimbi amesema bado Serikali inaendelea kuona namna ya kutafuta masoko ya mazao ya wakulima ili kuondokana na tatizo la upatikanaji wa masoko.
Dkt. Nchimbi pamoja na Timu alioyoongozana nayo akiwemo Mwenezi Taifa, Amos Makalla wapo mkoani Ruvuma kwa ziara ya siku tano, ambapo anafanya mikutano ya ndani na mikutano ya hadhara pamoja na kutembelea huduma za jamii katika Wilaya za Songea, Mbinga na Nyasa.
More Stories
Tanzania kuwa mwenyeji Mkutano wa Kimataifa matumizi bora ya Nishati
Madiwani Ilala watoa chakula kwa watoto yatima
Waziri Mkuu: Tumieni matokeo ya tafiti za kisayansi katika utekelezaji wa mipango ya kitaifa