*Aahidi neema kwa wananchi wa Rorya na Tarime
Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online
MGOMBEA Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi,amewaahidi Wana-Rorya, kuwa chama hicho kitaendelea kuwaletea maendeleo ikiwo ujenzi wa zahanati 10,endapo kitaendelea kushika dola.

Dkt. Nchimbi ameyasema hayo,Oktoba 31, 2025,wilayani Rorya mkoani Mara, wakati akihutubia wananchi, ikiwa ni muendelezo wa kampeni za CCM zinazoendelea nchini.
Amesema pia kitajenga vituo vya afya vipya vitano, kuongea watumishi wapya 150 kwenye sekta ya afya, ujenzi wa shule mpya 10 za sekondari,shule za mshingi tano, upatikanaji wa umeme kwa vitongoji vyote, upatikanaji wa maji kwa asilimia 95, ujenzi wa majosho 19, vizimba 300 na mabwawa 100.
Sambamba na hayo, wakati akiendelea kunadi sera za CCM kwa miaka mitano ijayo, akohutubia wananchi wa Nyamongo, Wilaya ya Tarime Vijijini mkoani Mara, amesema, katika kipindi cha miaka mitano ijayo, kati ya maendeleo yatakayofanywa katika Wilaya hiyo ni kuwa ni pamoja na vituo vya afya kufikia 20,zahanati 70, upatikanaji wa maji kwa asilimia 95.
Vingine ni ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kutoka Tarime hadi Mugumu yenye urefu wa Km 87, Mogabiri hadi Nyamongo Km 25, Tarime hadi Mogabiri Km 9.3 na Nyamongo hadi Mugumu Km 45.
Pia Dkt. Nchimbi amewaambia wakazi wa Nyamongo kuwa, ipo sababu ya kuendelea kukichagua chama hicho kutokana na kazi kubwa iliyofanywa ya kuwaletea maendeleo.

Huku akisema kuwa, katika miaka mitano iliyopita Jimbo hilo limepata mafanikio makubwa kama vile ongezeko la vituo vya afya kutoka 6 hadi 11, zahanati kutoka 31 hadi 50, shule za msingi kutoka 137 hadi 162, sekondari kutoka 38 hadi 54 na upatikanaji wa maji umeongezeka kutoka asilimia 51 hadi 73 na umeme vijijini kutoka 68 hadi 88.


More Stories
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI
Wananchi Dodoma washauri TBA kujenga nyumba za kupangisha watu binafsi