Na Mwandishi Wetu, TimesMajira,Online Zanzibar
MGOMBEA Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Hussein Mwinyi, amesema Serikali imefanya kazi kubwa katika sekta ya miundombinu na huduma za utalii, lakini kuna mambo ambayo hayajafanikiwa, hivyo ameahidi kuyashughulikie ikiwamo tatizo la maji.
Ameahidi kushughulikia tatizo hilo ili watu wote wapate maji ikiwemo maeneo ya uwekezaji wa utalii.
Dkt. Mwingi alitoa ahadi hiyo jana kwenye mkutano wake mkubwa wa kampeni uliofanyika Nungwi. “Chamgamoto la pili ni tatizo la utalii kutonufaisha wazawa na wajasiriami wadogo wa mboga na hakuna soko la uhakika, tutahakikisha sasa kipaumbele ni kwa wazawa,” alisema Dkt. Mwinyi na kuongeza;
“Tutatoa kipaumbele kwa kutoa ujuzi kama elimu ya ufundi na mahoteli ili waajirike na wajiajiri.”
Pia alisema kuna tatizo la wajasiriamali wadogo ni masoko. Alisema sehemu kubwa wavuvi wa Kaskazini Unguja wanakabiliwa na zana za kisasa kushindwa kuvua bahari kuu na moja ya sekta ya uchumi blue ni uvuvi.
“Tutaweka viwanda vya kusindika samaki na masoko ya mazao yao. Kuna tatizo la barabara za lami, sehemu kubwa ya barabara kuu zina lami sasa barabara za ndani za kusafirisha watalii na wenyeji tutahakikisha kazi inakua kumalizia,”alisema.
Kwa upande wa migogoro ya ardhi hasa katika maeneo ya wawekezaji, kushirikiana na viongozi kupora maeneo yao. “Suala la ardhi ni rasilimali inayotakiwa kunufaisha wenyeji na wawekezaji kupata haki stahiki,” alisema Dkt. Mwinyi.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dkt. Ali Mohammed Shein, amesema nafasi ya urais si ya kubahatisha, bali lazima ishikwe na mtu mwenye sifa za kuhimili maendeleo na ustawi wa nchi kama alivyo mgombea wa CCM Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi.
Dkt. Shein aliyasema hayo jana alipokua akimnadi Dkt. Mwinyi, katika mkutano huo wa kampeni uliofanyika Nungwi, mkoa wa Kaskazini Unguja.
Akikumbushia alipopita Nungwi kuomba kura alipokua mgombea Urais na kushinda, Dkt. Shein alisema urais ni nafasi kubwa na nzito ya kuwatumikia wananchi na si ya kufanya majaribio.
Alisema yeye na marais wa CCM waliotangulia hawajana mwenye sifa kama Dkt. Mwinyi katika orodha ya wagombea wengine. Akipokewa na wimbo wa taarab wa “mpewa hapokonyeki aliyepewa kapewa”, Dkt. Shein amesema “In Shaa Allah Dkt. Hussein atapewa na hakuna wa kumpokonya na kuwaomba wananchi wa Zanzibar kumpa kura nyingi mgombea wa Urais wa CCM Zanzibar na wagombea wa nafasi nyingine za ubunge, uwakilishi na udiwani.
Watu wafurika
Mkutano huo wa kampeni umehudhuriwa maelfu ya wananchi wengi wao wakiwa wenyeji wa Nungwi na Mkoa Kaskazini Unguja. Walisema hawajawahi kuona umati mkubwa wa watu uliojitomeza katika mkutano huo.
“Hakuna pahala pa kuweka hata mguu, watu ni wengi sana kike, kiume,”alisema Ame Silima Mkazi wa Kidoti.
Mkazi mwengine wa Nungwi alisema idadi kubwa ya watu waliohudhuria katika mkutano huo ni uthibitisho wa kukubalika na kuungwa mkono kwa Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM, Dkt Hussein Ali Mwinyi.
Viongozi wengine waliohudhuria mkutano huo ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, Mwenyekiti mstaafu wa CCM Taifa na Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi. Wengine ni Waziri Kiongozi mstaafu, Shamsi Vuai Nahodha.
More Stories
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba
27 kulipwa kifuta jasho Nkasi
Mwakilishi Mkazi wa UN nchini awasilisha hati