December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Dkt.Mpango kuweka Jiwe la Msingi kipande Cha Tabora -Isaka

Na David John, timesmajiraonline

MAKAMU wa Rais ,Dkt. Philip Mpango anatarajia kuweka jiwe la msingi la Reli ya kisasa ya SGR Tabora _Isaka ambapo mradi huo utakuwa ni kuhitimisha awamu ya kwanza ya mradi kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza .

Mradi huo wa SGR Tabora _Isaka utahusisha ujenzi wa reli yenye kiwango cha kimataifa SGR Kwa urefu wa kilomita 165 ikijumuisha kilomita 130 njia kuu na kilomita 35 za njia za kupishana .

Akizungumza mbele ya waandishi wa Habari Mkurugenzi mkuu wa shirika la TRC Madogosa Masanja Januari 16 mwaka 2023 Mkoani Shinyanga Wilaya ya kahama ndani ya halmashauri ya Msalala amesema mradi wa SGR kipande cha Tabora _Isaka ni utekelezaji wa awamu ya kwanza ya mradi wa SGR Dar es Salaam _Mwanza ( km 1,219) yenye vipande vitano Dar es Salaam -Morogoro ,Morogoro -Makotopora .

Masanja ameongeza kuwa kipande kingine ni Makotopora -Tabora ,Tabora -Isaka na Isaka-hadi kufika Mwanza na ujenzi wa reli hiyo ya kisasa utaendelea kuleta faida Kwa wananchi na taifa Kwa ujumla ikiwemo upatikanaji wa fursa za Moja Kwa Moja kupitia Kampuni ,wajasiriamali wadogo na biashara .

Shirika la reli Tanzania limeandaa treni mbili maalumu siku ya Januari 18 2023 itakayobeba wananchi kutoka stesheni ya Tabora saa 11:00 asubuhi na kutoka Shinyanga saa 12 : 00 asubuhi kuelekea Isaka na baadae kurudi Tabora na Shinyanga baada hafla kuisha .

Shirika hilo linawakaribisha wananchi wote hususani Kanda ya ziwa kuhudhuria tukio hilo la kihistoria la uwekaji wa jiwe la msingi .