Na Esther Macha, Timesmajira Online, Mbeya
IMEELEZWA kuwa watu wenye ulemavu wanaonekana kusahaulika katika jamii kwenye masuala muhimu ikiwemo afya, elimu na mambo mengine ya msingi hivyo kundi hilo kuwa hatarishi kwa magonjwa ya kuambukiza.
Akizungumza na waandishi wa habari leo katika eneo la maegesho la hospitali hiyo Mkuu wa huduma za Tiba na uongozi uchunguzi, Dkt. Uwesu Mchepange wakati wa maadhimisho ya siku ya Homa Ini Duniani, amesema kuwa kundi la watu wenye ulemavu lipo kwenye hatari kubwa ya kuambukiza homa ya Ini.
Dkt. Mchepange amesema kuwa katika maadhimisho hayo wameona vema kulenga kundi la watu wenye ulemavu kwasababu kundi hilo limesahaulika kwenye jamii katika mambo mbalimbali ya msingi.
Hata hivyo amesema kuwa kundi hilo lipo kwenye hatari kubwa kwenye magonjwa ya kuambukiza kwani baadhi ya watu wamekuwa wakilitumia kundi la watu wenye ulemavu katika faida ili kufanya mambo yao ambayo yanaweza kulifanya kundi hilo kupata magonjwa ya kuambukiza.
Aidha amesema katika takwimu za mwaka 2021 zaidi ya watu mil.1 wanapoteza maisha kila mwaka kutokana na homa ya Ini duniani au vitu ambavyo vinavyoambatana na homa ya ini kwa maana madhara mbali mbali yanayotokana na homa ya Ini .
Amesema kuwa inakadiriwa asilimia 4.4 ya watanzania wanaambukizi ya virusi vya homa ya Ini lakini mbaya zaidi watu wamekuwa wakiogopa virusi vya ukimwi kuliko virusi vya homa ya Ini wakati virusi vya homa ya Ini ni hatari zaidi kuliko ukimwi hatari yake inatokana na kwamba uwezo wa kuambukiza virusi vya homa ya Ini mkubwa zaidi kuliko virusi vya ukimwi ndo sababu ya kuliona kundi hili watu wenye ulemavu kulipa kipaumbele katika maadhimisho haya.
“Na unapozungumzia homa ya Ini hasa hii inayosabishwa na virusi hii inaambukiza kwa njia mbalimbali ambapo njia kuu ni zile zile ambazo zinaambukiza virusi vya ukimwi” amesema Dkt. Mchepange.
Akifafanua zaidi Mkuu wa huduma za uchunguzi hospitali ya Rufaa ya kanda ya Mbeya amesema kuwa njia za maambukizi kuu ni ngono zembe haina kinga yeyote,maambukizi ya mama kwenda kwa mtoto,kupitia damu ambayo ni sindano kwa wale wanaojidunga kwenye madawa ya kulevya na kwamba hizo njia kuu.
Hata hivyo Dkt. Mchepange amesema kuwa ndo sababu kuu walioona kuwa kundi la watu wenye ulemavu limekuwa likiachwa nyuma kwenye mambo mengi lakini pia lipo kwenye hatari ya kupata maambukizi ya homa ya Ini hivyo wakaona upo muhimu wa kulisaidia kundi hilo watu wenye ulemavu kupata elimu ,upimaji na chanjo ya homa ya Ini kwa walemavu .
Dkt.Peter Kishimbo Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Ndani amesema kuwa magonjwa ya homa ya Ini yanaambukizwa kwa ngono zembe ,njia ya damu ,kwa mama kwenda kwa mtoto ,vitu vyenye ncha kali na kwamba dalili za homa ya Ini njano kwenye macho ,homa,tumbo kuuma upande wa kulia, viungo kuuma ,kuharisha na kutapika.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha watu wenye ulemavu mkoa wa Mbeya ,Juma Mwampepo amesema kuwa wanashukuru hospitali ya Rufaa kanda ya Mbeya kwa kutambua umuhimu wa kundi la watu wenye ulemavu ili kupata elimu ya homa ya Ini kwasababu wengi wao walikuwa hawaifahamu hivyo wamefumbuliwa macho na kupata somo kubwa.
Aidha Mwampepo amesema kuwa hospitali ya Rufaa imeweka mtu ambaye anashugulika na watu wenye ulemavu hivyo tunaomba idara zingine za serikali zingekuwa zinafanya kamna ambavyo hospitali ya rufaa inafanya changamoto za watu wenye ulemavu zingepungua au kuisha.
Nathael Mwasamkinga ni Mwenyekiti wa wagonjwa wa afya ya akili ,amesema kuwa wagonjwa wa akili ni mgonjwa anayezaliwa akiwa mzima lakini anakuja kupata athari ya kunywa maji machafu na hivyo kupata athari hivyo ameomba wananchi kutowaficha watoto au watu wazima wote hao wanahitaji huduma hivyo wanapaswa kusaidiwa na watu wazima wanatakiwa kuwa wasemaji wa watoto hao.
“Tuwe wasemaji wa wagonjwa wa afya ya akili sababu hawana uwezo wa kujieleza na tulio wazima tuwe msaada mkubwa kwani ni watu muhimu sema wanakosa watu wa kuwasemea,hawa watu wamesaulika sana kwenye Taifa hili “amesema Mwenyekiti huyo.
More Stories
Serikali kupeleka mawasiliano maeneo ya mipakaniÂ
Sekondari ya Butata mbioni kufunguliwa Musoma Vijijini
TIC yapongeza mradi wa Kampuni ya Big Best