Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma
MBUNGE wa Same Magharibi (CCM) Dkt.David Mathayo Rais Dkt.Samia amestahili kupitishwa kuwa mgombea pekee wa kiti Cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwani amefanya mambo mengi ya maendeleo hapa nchini katika sekta zote ikiwemo na utekelezaji wa miradi ya kimkakati.
Akizungumza jijini Dodoma baada ya jina la Dkt .Samia kupitishwa kuwa mgombea pekee wa nafasi hiyo na Dkt.Hussein Mwinyi kupitishwa kuwa mgombea pekee wa kiti Cha Urais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Dkt.Mathayo amesema hatua hiyo ndiyo imewafanya wajumbe kupitisha majina yao kwa dhati Ili wapate nafasi ya kuendeleza mazuri yote katika kuleta maendeleo nchini.
“Ni kawaida ya Chama chetu hiki na kwa jinsi tulivyozoea, mgombea Urais anapewa tena nafasi ya pili ili amalizie miaka yake 10 madarakani,
lakini hiyo tu haitoshi mama Samia na Dkt Mwinyi wamefanya kazi kubwa ya kuleta maendeleo kwa muda mfupi sana ,
“Sasa kwa kazi waliyoifanya kwa miaka minne tunatamani waongezewe miaka mingine mitano wafanye zaidi ya haya waliyoyafanya,kwa hiyo sisi Leo kusema kwamba tunapitisha jina lake kwanza ni kazi ya Mkutano Mkuu kufanya hivyo,
“Lakini kazi zao walizozifanya kwa miaka minne, zimetufanya wajumbe tumesisimkwa na kutufanya tuone kuna haja gani ya kuhangaika kusema labda tusubiri kuja kuwapitisha baadaye wakati wamefanya kazi nzuri na hatutegemei kukuta mwenye rekodi nzuri itakayompita Samia .”amesema Dkt.Mathayo
Akimzungumzia Makamu Mwenyekiti Bara Stephen Wasira Dkt Mathayo wana-CCM wamepata jembe, mpambanaji na mtu atakayekisaidia chama hicho.
“Wasira akiwa Waziri wa Kilimo na Mimi nikiwa Naibu wake huko miaka ya nyuma,alinifanya niwe kiongozi mzuri sana, alikuwa mwadilifu na alikuwa Waziri mwenye akili sana ,Mimi nilimwita dictionary inayotembea,
“Kwa hiyo hata alivyotajwa kuwa ndiye anashika nafasi hiyo ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara ,sikuona ajabu , hata hivyo naona amechelewa kushika nafasi hiyo “amesema
Mbunge huyo amesema Wasira ni mtu anayejua kujenga hoja,ana uzoefu mkubwa katika masuala ya Uongozi na anapenda haki na uzalendo wa nchi yake.
Aidha Dkt.Mathayo amezungumzia kwa uchache aliyoyafanya katika Jimbo lake la Same Magharibi huku akisema amewaombea wananchi wake maendeleo kwa Dkt.Samia na yamepatikana katika sekta mbalimbali.
Lakini pia amesema,kwa fedha zake binafsi akiwa kama Mbunge , ametoa mchango mkubwa sana kusaidia maendeleo ya wananchi jimboni humo na hivyo anaamini atapita tena katika Uchaguzi ujao wa 2025 Ili apate nafasi ya kuleta maendeleo zaidi.
“Uzuri wa wananchi ukiwafanyia mambo mazuri ya kuwaletea maendeleo wanashukuru,kwa hiyo Mimi naamini watanichagua tena”amesema Dkt Mathayo
Akizungumza kwa uchache aliyoyafanya katika Jimbo Hilo amesema ni pamoja na kutoa mabomba kwa ajili ya kusambaza huduma ya maji yenye thamani ya zaidi ya sh.300 milioni lakini pia mwishoni mwa Disemba mwaka jana amesaidia saruji na Mabati kumalizia zahanati ,na kusaidia wananchi kumalizia ujenzi wa misikiti na makanisa ili watu wapate sehemu za kumwabudu Mungu.
More Stories
Wanafunzi 3000 wenye uhitaji wapatiwa vifaa vya shule
Rais Samia, Mwinyi ‘mitano tena’ Nchimbi aula
Dkt.Kikwete:Ushindi wa CCM ni lazima