Na Esther Macha, Timesmajira Online, Mbeya
JAMII mkoani Mbeya imetakiwa kuachana na vitendo vya chuki ili kuendelea kudumisha amani ya nchi na kuondokana na vitendo vya ukatili vinavyosababisha mauaji.
Wito huo umetolewa jijini Mbeya na Mkurugenzi Mtendaji wa shirika lisilokuwa la kiserikali la ‘Family Vibes Foundation’ Dkr. Mayrose Majinge wakati akitoa taarifa Kwa wanahabari kuhusu uzinduzi wa kampeni ya ‘Zuia Chuki, Tumia 4R furahia maisha ambao unatarajia kufanyika Juni Mosi,2024 katika chuo kikuu cha katoliki Mbeya (CUoM).
Amesema kwenye utafiti walioufanya wamegundua kuwa katika ulimwengu wa chuki kuna matukio ya uvunjifu wa amani na watu kijichukulia Sheria mkononi Kwa sababu ya kuweka chuki kwenye mioyo yao.
Dkt..Majinge amesema chuki ni ugonjwa wenye sumu Kali na unaoenea kwa kasi ya ajabu na unasababisha vifo kuliko magonjwa mengine, akieleza kuwa walimwengu wanahitaji kufanya kila njia ili kuepuka chuki Kwa ajili ya usalama wa kiafya, kiuchumi, kifamilia, kitaifa na kimataifa.
“Chuki iko chini ya kategoria ya hisia, kama zilivyo hisia nyingine inaweza kuwa chanya au hasi kulingana na jinsi inavyotumiwa, Kwa mfano kuchukia Rushwa au vurugu ni matumizi mazuri, huku ubaguzi wa rangi, kutovumiliana Kwa kidini au unyanyasaji wa kijinsia ni matumizi mabaya”
Kwa mujibu wa Dkt.Majinge amesema lengo la kampeni ni kuwezesha misheni ya kukabiliana na chuki ulimwenguni yenye uenezaji wa elimu juu ya kulinda afya Bora,utu wa mtu na maendeleo binafsi na jamii Kwa ujumla.
More Stories
Zaidi ya wananchi 32,000 Vijiji vya Wilaya za Morogoro na Mvomero kuanza kupata mawasiliano
Wafanyabiashara waomba elimu ya namna watakavyorejea soko kuu
DCEA,Vyombo vya Ulinzi na Usalama vyafanya operesheni ya kihistoria