April 19, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Dkt.Kimei atajwa kuwa kinara wa kuzungumzia mahitaji ya wananchi

Na Mwandishi Wetu,Dodomaa

MBUNGE wa Jimbo la Vunjo Dkt Charles Kimei ametajwa kuwa kinara wa kuzungumzia mahitaji ya wananchi kwa kuwa miongoni mwa wabunge vinara wa kusema, kuchangia au kuhoji katika kila kikao cha bunge la 12 linalotarajiwa kuvunjwa mwishoni mwa mwezi Juni mwaka huu.

Kwa mujibu wa tovuti ya Bunge la Tanzania inaonyesha Dk.Kimei amechangia mara 49 na kuuliza maswali 110 yanayohusu jimboni na yanayogusa Taifa kwa ujumla.

Mbunge huyo ni aina ya viongozi wanaoipenda kazi yao na kuguswa ambao wamekuwa wakioonekana katika majimbo yao wakifanya mikutano ya wananchi kutoa mrejesho, kusikiliza na kutatua kero pamoja na ziara za ukaguzi wa miradi ya maendeleo.