Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online-Dar
RAIS Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Jakaya Kikwete,amewapigia chapuo wagombea wa Chama Cha Mapindizi(CCM),akiwemo mgombea Ubunge Jimbo la Kivule Ojambi Masaburi na Urais Dkt.Samia Suluhu Hassan,kwa wananchi ili waweze kuwapigia kura katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 29 mwaka huu.
Dkt.Kikwete,akizungumza katika uzinduzi wa kampeni za jimbo la Kivule,amesema,wagombea wa CCM ndio wanaweza kuwaletea maendeleo hivyo kura za ndio wazielekeze kwao.
Pia amesema,Dkt.Samia ameimarisha mapato ya nchi na kujenga uhusiano wa kimataifa na amegusa maisha ya watu wote ikiwemo sekta ya afya ambapo wajawazito wanajifungua kwa uhakika hali ilichangia kupunguza vifo vya mama na mtoto.
Kwa upande wakegombea Ubunge Jimbo la Tarime Vijijini,Mwita Waitara,amewahimiza wananchi wa Jimbo la Kivule na wenyeji wa Tarime wanaoishi jimboni humo kumpigia kura Ojambi Masaburi na Dkt.Samia Suluhu Hassan na madiwani wa chama hicho ili waweze kuleta maendeleo.
Naye mgombea Ubunge Jimbo Kivule kupitia CCM,Ojambi Masaburi,amesema uwezo wa kuongoza Jimbo hilo nakuwaletea wananchi maendeleo anao.
Masaburi amesema wakati akiwa Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar-es-Salaam ameshirikiana na madiwani wa jiji hilo kuleta maendeleo wilayani Ilala ikiwemo ujenxi wa vituo vya afya kwa Kata zote za Jimbo la Kivule.
Ujenzi wa tanki kubwa la maji la Bangulo,ujenzi wa barabara Kitunda-Kivule kwenda Msongola umeanza kwa kiwango cha lami.
Huku barabara zingine zinazojengwa kwa kiwango cha lami ni Pugu-Majohe-Viwege,Nyangaza-Majohe-Moshi Bar-,Machimbo Matembele,shule ya Misitu- ,Hospitali ya Wilaya Kivule,Picha ya Ndege Kanisa la Roma .

More Stories
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI
Wananchi Dodoma washauri TBA kujenga nyumba za kupangisha watu binafsi