January 20, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Dkt. Kikwete amjulia hali Msama

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Rais Mstaafu wa awamu ya nne Mhe. Dkt Jakaya Mrisho kikwete amemtakia afya njema mfanyabiashara maarufu ambaye ni Mkurugenzi wa Msama Promotions na Dira media group Alex Msama baada ya siku chache kuugua ghafla na kulazwa katika Taaisis ya Moyo ya Jakaya Kikwete,JKCI kabla ya sasa kuhamishiwa Moi kwa matibabu zaidi.

Kwa mujibu wa watu wa karibu wa Alex Msama Rais Kikwete amemtakia afya njema ili aweze kupona Mkurugenzi huyo tayari kwa ajili ya kuendelea na shughuli zake za kujenga nchi,ambazo amekuwa akizifanya kila msama kwasasa anaendelea na matibabu katika hospital ya moi hapa dsm