April 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Dkt Joyce: Ukatili wa kijinsia wazidi kuongezeka, waingia ukatili wa mitandao

Judith Ferdinand, Morogoro

Imeelezwa kuwa ukatili wa kijinsia umezidi kapanuka ambapo kwa sasa umeingia ukatili wa mitandao.

Huku teknolojia ikiwa imebadilika hivyo ni vizuri waandishi wa habari kuendelea kupewa mafunzo ili waweze kuwa na uelewa mpana juu ya masuala ya ukatili yatakayowasaidia katika utendaji kazi wao.

Hayo yamebainishwa na Mtaalamu wa Mawasiliano ya Umma,Mratibu wa Programu ya Women in News nchini Tanzania,Dkt.Joyce Bazira wakati wa mafunzo ya siku mbili kwa waandishi wa habari 20 kutoka mikoa na vyombo mbalimbali nchini.

Mafunzo hayo yaliyofanyika mkoani Morogoro yalioandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) kwa ufadhili wa UNESCO.

Dkt.Bazira amesema,mafunzo ya ukatili wa kinjisia kwa wanawake na watoto ni muhimu kwa waandishi wa habari,kwa sababu ni chombo kinachowainganisha wananchi na mamlaka.

Amesema,mafunzo kama hayo ya kuwajengea uwezo yanawasaidia sana,kwa sababu wanapata mbinu,ujuzi na maarifa ambapo wanafundishwa pia namna gani wanaweza kuandika habari ambazo zitaongeza uelewa kwa wananchi juu ya masuala ya ukatili.

“Nadhani kuwa na ujuzi,maarifa na kujiendeleza ni jambo muhimu sababu ukatili wa kijinsia kwa watoto na wanawake ni kitu kinachozidi kupanuka,sasa hivi umeingia mpaka ukatili wa kwenye mitandao,”.

“Teknolojia imebadilika hivyo ni vizuri waandishi wa habari kuendelea kupewa mafunzo ili waweze kuwa na uelewa mpana juu ya masuala ya ukatili,”amesema Dkt.Bazira.

Pia amesema, waandishi wa habari wanapaswa kuwa na jicho la tatu kwa kuibua na kuchimba mambo kiundani.

Kwa upande wake mmmoja wa waandishi wa habari waliohudhuria mafunzo hayo,Mary Geofrey,amesema ameshukuru TAMWA na UNESCO kwa kuwapa mafunzo hayo,hivyo anaamini kwa kiasi kikubwa yanaenda kuwavusha kwa hatua moja kwenda nyingine kama waandishi wa habari ambao wamekuwa tukifipoti masuala ya kijinsia.

“Bado kuna mwanya(gap)mkubwa kwani matukio ya ukatili yanaendelea kwenye jamii,kupitia mafunzo haya tunaamini tunaenda kuwa watu wapya na kuripoti matukio ya ukatili na kuangalia chanzo ili yaweze kumalizika katika jamii zetu,”.

“Ni jukumu letu kwenda kuchimba habari kama hizi,kutoa elimu kwa jamii na kuwa mabalozi kwa kuonya,kuelimisha,kufundisha na siyo kuishia tu kuripoti habari ili kumaliza tatizo hili nchini hapa,”amesema Mary.

Naye Sudi Jongo, amesema jambo muhimu kwa TAMWA kama taasisi na taasisi zingine ambazo zimekuwa zikihamasisha masuala ya jinsia kuendelea kuwatumia wanahabari na vyombo vya habari.

Hata hivyo Mchumi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Seto Ojwando ameelezea utekelezaji wa mpango wa taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Amesema, Tanzania imeendelea kutekeleza mpango kazi wa taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto(MTAKUWWA 2017/18-2021/22),kupitia maeneo makuu 8 ya utekelezaji kwa lengo la kuimarisha ulinzi,haki na ustawi wa wanawake na watoto.

“Vitendo vya ukatili katika jamii huathiri zaidia wanawake na watoto,lengo kuu la MTAKUWWA ni kupunguza aina zote za ukatili dhidi ya wanawake na watoto kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2022.

Pia amesema,katika kukabiliana na changamoto ya ukatili vyombo vya habari vina wajibu wa kuendelea kutoa elimu kwa jamii ili kuondokana na mila na desturi zinazochochea vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Mtaalamu wa Mawasiliano ya Umma, Dkt.Joyce Bazira,wakati akizungumza na waandishi wa habari (hawapo) pichani baada ya kumalizika kwa mafunzo siku mbili ya kuwajengea uwezo juu ya masuala ya ukatili wa waandishi wa habari kutoka mikoa na vyombo mbalimbali nchini, yaliyofanyika mkoani Morogoro yalioandaliwa na TAMWA kwa ufadhili wa UNESCO.picha na Judith Ferdinand

Baadhi ya waandishi wa habari waliopata fursa ya kushiriki mafunzo siku mbili ya kuwajengea uwezo juu ya masuala ya ukatili wa waandishi wa habari kutoka mikoa na vyombo mbalimbali nchini, yaliyofanyika mkoani Morogoro yalioandaliwa na TAMWA kwa ufadhili wa UNESCO,wakiwa katika majadiliano.picha na Judith Ferdinand

Baadhi ya waandishi wa habari waliopata fursa ya kushiriki mafunzo siku mbili ya kuwajengea uwezo juu ya masuala ya ukatili wa waandishi wa habari kutoka mikoa na vyombo mbalimbali nchini, yaliyofanyika mkoani Morogoro yalioandaliwa na TAMWA kwa ufadhili wa UNESCO,wakiwa katika majadiliano.picha na Judith Ferdinand

Mtaalamu wa Mawasiliano ya Umma, Dkt.Joyce Bazira(wa kwanza kushoto walioka) huku katikati akiwa ni Mchumi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Seto Ojwando wakiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari kutoka mikoa na vyombo mbalimbali nchini,waliopata fursa ya kushiriki mafunzo ya siku mbili ya kuwajengea uwezo juu ya masuala ya ukatili,yaliyofanyika mkoani Morogoro yalioandaliwa na TAMWA kwa ufadhili wa UNESCO.picha na Judith Ferdinand
Mtaalamu wa Mawasiliano ya Umma, Dkt.Joyce Bazira,wakati akitoa mafunzo siku mbili ya kuwajengea uwezo juu ya masuala ya ukatili wa waandishi wa habari kutoka mikoa na vyombo mbalimbali nchini, yaliyofanyika mkoani Morogoro yalioandaliwa na TAMWA kwa ufadhili wa UNESCO.picha na Judith Ferdinand