Judith Ferdinand, Morogoro
Imeelezwa kuwa ukatili wa kijinsia umezidi kapanuka ambapo kwa sasa umeingia ukatili wa mitandao.
Huku teknolojia ikiwa imebadilika hivyo ni vizuri waandishi wa habari kuendelea kupewa mafunzo ili waweze kuwa na uelewa mpana juu ya masuala ya ukatili yatakayowasaidia katika utendaji kazi wao.
Hayo yamebainishwa na Mtaalamu wa Mawasiliano ya Umma,Mratibu wa Programu ya Women in News nchini Tanzania,Dkt.Joyce Bazira wakati wa mafunzo ya siku mbili kwa waandishi wa habari 20 kutoka mikoa na vyombo mbalimbali nchini.
Mafunzo hayo yaliyofanyika mkoani Morogoro yalioandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) kwa ufadhili wa UNESCO.
Dkt.Bazira amesema,mafunzo ya ukatili wa kinjisia kwa wanawake na watoto ni muhimu kwa waandishi wa habari,kwa sababu ni chombo kinachowainganisha wananchi na mamlaka.
Amesema,mafunzo kama hayo ya kuwajengea uwezo yanawasaidia sana,kwa sababu wanapata mbinu,ujuzi na maarifa ambapo wanafundishwa pia namna gani wanaweza kuandika habari ambazo zitaongeza uelewa kwa wananchi juu ya masuala ya ukatili.
“Nadhani kuwa na ujuzi,maarifa na kujiendeleza ni jambo muhimu sababu ukatili wa kijinsia kwa watoto na wanawake ni kitu kinachozidi kupanuka,sasa hivi umeingia mpaka ukatili wa kwenye mitandao,”.
“Teknolojia imebadilika hivyo ni vizuri waandishi wa habari kuendelea kupewa mafunzo ili waweze kuwa na uelewa mpana juu ya masuala ya ukatili,”amesema Dkt.Bazira.
Pia amesema, waandishi wa habari wanapaswa kuwa na jicho la tatu kwa kuibua na kuchimba mambo kiundani.
Kwa upande wake mmmoja wa waandishi wa habari waliohudhuria mafunzo hayo,Mary Geofrey,amesema ameshukuru TAMWA na UNESCO kwa kuwapa mafunzo hayo,hivyo anaamini kwa kiasi kikubwa yanaenda kuwavusha kwa hatua moja kwenda nyingine kama waandishi wa habari ambao wamekuwa tukifipoti masuala ya kijinsia.
“Bado kuna mwanya(gap)mkubwa kwani matukio ya ukatili yanaendelea kwenye jamii,kupitia mafunzo haya tunaamini tunaenda kuwa watu wapya na kuripoti matukio ya ukatili na kuangalia chanzo ili yaweze kumalizika katika jamii zetu,”.
“Ni jukumu letu kwenda kuchimba habari kama hizi,kutoa elimu kwa jamii na kuwa mabalozi kwa kuonya,kuelimisha,kufundisha na siyo kuishia tu kuripoti habari ili kumaliza tatizo hili nchini hapa,”amesema Mary.
Naye Sudi Jongo, amesema jambo muhimu kwa TAMWA kama taasisi na taasisi zingine ambazo zimekuwa zikihamasisha masuala ya jinsia kuendelea kuwatumia wanahabari na vyombo vya habari.
Hata hivyo Mchumi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Seto Ojwando ameelezea utekelezaji wa mpango wa taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Amesema, Tanzania imeendelea kutekeleza mpango kazi wa taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto(MTAKUWWA 2017/18-2021/22),kupitia maeneo makuu 8 ya utekelezaji kwa lengo la kuimarisha ulinzi,haki na ustawi wa wanawake na watoto.
“Vitendo vya ukatili katika jamii huathiri zaidia wanawake na watoto,lengo kuu la MTAKUWWA ni kupunguza aina zote za ukatili dhidi ya wanawake na watoto kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2022.
Pia amesema,katika kukabiliana na changamoto ya ukatili vyombo vya habari vina wajibu wa kuendelea kutoa elimu kwa jamii ili kuondokana na mila na desturi zinazochochea vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
More Stories
DC Korogwe awataka viongozi wa vijiji kuwatumikia wananchi kwa uadilifu
Premier Bet yamtangaza mshindi mkubwa
Dkt. Kazungu atembelea miradi ya umeme Dar es Salaam