Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma
WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum Dkt.Dorothy Gwajima amewaagiza Maafisa Maendeleo na Maafisa Ustawi wa Jamii kuhakikisha agenda ya Malezi ,Makuzi na Maendeleo ya awali ya Mtoto (MMMAM) inazungumzwa katika ngazi zote kwenye maeneo yao kwa lengo la kuelimisha jamii.
Waziri Dkt.Gwajima ametoa kauli hiyo jijini Dodoma wakati akifungua mkutano wa Kitaifa wa Wadau watekelezaji wa Programu Jumuishi ya Kitaifa ya Malezi ,Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT-MMMAM 2021/22-2025/26) inayolenga watoto kuanzia umri wa miaka sifuri hadi minane ili wawe na ukuaji timilifu.
Amesema ili kuhakikisha utekelezaji wa Programu hiyo unafanywa hadi na mwananchi mmoja mmoja ni lazima maaafisa hao watumie majukwaa,mitandao yao ya kijamii pamoja na mikutano yote kufikisha ujumbe huo kwa jamii ambao una maslahi mapana kwa watoto na Taifa kwa ujumla.
Aidha amewataka kuhakikisha baada ya kujengewa uwezo kwenye mafunzo hayo wanakwenda kumairisha majukwaa mbalimbali ya kuelimisha jamii kuhusu Programu ya MMMAM na utekelezaji wake.
Lakini pia amewataka maafisa hao wakaimarishe uratibu wa MMMAM kwa ngazi za mikoa na halmashauri ili programu hii ilete matokeo chanya lakini pia waongelee malezi na makuzi kama kipaumbele kwenye mbaraza yao kuanzia kwenye vijiji hadi kata.
Aidha amewataka Makatibu Tawala wasaidizi wa mikoa wahakikishe afua za malezi makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto zinaingizwa kwenye bajeti za halmashauri na kwamba mwakani anataka kuona bajeti kwenye halmashauri na mikoa katika utekelezaji wa Programu hiyo.
“Tutakuwa tunafuatilia hilo kuona halmashauri zilizoingiza kwenye mijadala yao suala la MMMAM ili tuone namna gani PJT-MMMAM inavyozingatiwa katika utekelezaji wake.”amesema Dkt.Gwajima
Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Children in Crossfire (CiC) linaloshughulika na watoto Creig Ferla amesema,kipaumbele cha utekelezaji wa Programu ni kuanzia ngazi za juu hadi kwa mtoto mmoja mmoja kwa lengo la kuhakikisha watoto wanakua kwa utimilifu wao.
“Kwa mujibu wa Sensa ya 2022 .iliyofanyika hapa nchini watoto wenye umri wa kuanzia sifuri mpaka miaka minane wapo asilimia 27 ya watanzania wote,kwa maana kwamba sura ya Taifa ,kati ya watanzania wanne mmoja ni wa umri wa miaka sifuri hjadi minane sawa na watanzania milioni 16,
“Sasas hao watoto milioni 16 ni nguvu kazi kubwa kwa Taifa hili na wote hao wakikua kwa utimilifu wao wanakwenda kuchagiza uchumi na maendeleo ya Taifa kwa kiasi kikubwa sana.”amesema Creig
Awali Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Mtandao wa Malezi,Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (TECDEN) Bruno Humpy amesema,wadau waliokutana ni Asasi 26 kutoka nchi nzima ambao wote kwa pamoja wanakwenda kuchagiza utekelezaji wa PJT-MMMAM katika mikoa yao kupitia mradi wa Mtoyto Kwanza.
“Mwanzoni tulianza na asasi za kiraia kutoka mikao 10,lakini leo tumechukua mikoa 16 iliyobaki,hawa wadau ni asasi ambao wanawezeshwa na TECDEN hivyo wanaenda kutekeleza mradi wa Mtoto Kwanza nchi nzima mradi ambao unachochea utekelezaji wa PJT-MMMAM.”amesisitiza Humpy
More Stories
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba
TRA kuongeza idadi ya waendesha uchumi walioidhinishwa
TRA Tanga wajivunia ukusanyaji mapato