December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Katibu wa CCM Wilaya ya Musoma Mjini, Ramadhani Dallo akimkabidhi Dokta Joachim Eyembe fomu ya kuomba kuteuliwa kuwania ubunge wa Jimbo la Musoma Mjini. (Picha na Fresha Kinasa).

Dkt.Eyembe awa wa 55 Musoma Mjini

Na Fresha Kinasa, TimesMajira Online, Mara

MGANGA Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara, Dkt. Joachim Eyembe amekuwa wa 55 kuchukua fomu ya kuomba kuteuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwania nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Musoma Mjini.

Dkt. Eyembe amesema, ameamua kuchukua fomu kutokana na msukumo wa Rais Magufuli kuwataka vijana kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi wa mwaka huu katika kuleta maendeleo kwa wananchi.

Amesema, akipata nafasi atahakikisha anatoa mchango wa maendeleo na kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi. ili kuungana na Rais Magufuli ambaye amelipaisha Taifa kiuchumi.

“Nikipata fursa ya kuchaguliwa nitatoa mchango wangu katika kuleta maendeleo kama ambavyo Rais Magufuli ametufanyia mambo makubwa Watanzania ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya barabara, reli na ununuzi wa ndege ambazo zimelitangaza na kuliheshimisha Taifa letu Kimataifa,”amesema.