January 25, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Dkt.Chana:Onesho la SITE ni fursa

Na Mwandishi wetu,timesmajira, Online

Wadau wa utalii wa ndani na nje ya nchi hususan Wakala wa Biashara za Utalii, watoa huduma za malazi, Wakala wa Safari na waongoza watalii wametakiwa kuchangamkia fursa za kiuchumi na kijamii zitakazotokana na Onesho la Swahili International Tourism Expo (SITE) litakalofanyika jijini Dar es salaam Oktoba 21 hadi 23, 2022.

Wito huo umetolewa na Waziri wa Maliasili na Utalii nchini,Balozi Dkt. Pindi Chana Jijini Arusha alipokua akizungumza na waandishi wa habari kuhusu onesho hilo la Sita litakalofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City, Jijini Dar es Salaam Tanzania.

Baadhi ya wadau wakimsikiliza Balozi Dkt.Pindi Chana kuhusu onesho hilo la Swahili International Tourism Expo (SITE) litakalofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City, Jijini Dar es Salaam.

“ Fursa hizo ni pamoja na kutangaza biashara, kutengeneza mtandao wa biashara na kutoa huduma mbalimbali wakati wa onesho, ni matarajio ya Serikali kuwa taasisi na makampuni mbalimbali mtajitokeza kwa wingi katika kufadhili shughuli mbalimbali ili kunufaika na fursa za kujitangaza kupitia onesho hili la S!TE” ameongeza Balozi Dkt. Chana alipokua akizungumza na waandishi wa habari kuhusu onesho hilo la Sita litakalofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City, Jijini Dar es Salaam Tanzania.

“ Fursa hizo ni pamoja na kutangaza biashara, kutengeneza mtandao wa biashara na kutoa huduma mbalimbali wakati wa onesho, ni matarajio ya Serikali kuwa taasisi na makampuni mbalimbali mtajitokeza kwa wingi katika kufadhili shughuli mbalimbali ili kunufaika na fursa za kujitangaza kupitia onesho hili la S!TE” Ameongeza Balozi Dkt. Chana