Na Irene Fundi, timesmajira
Waziri wa Madini, Dkt. Doto Biteko anatarajia kuwa mgeni rasmi katika mkutano wa madini unaotarajia kufanyika April 5 na 6,Mwaka huu katika ukumbi wa JNICC jijini Dar es Salaam.
Akizungumza leo na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Dkt. Venancee Mwasse,amesema Mkutano huo utahudhuriwa na watu zaidi ya 700 ukiongozwa na kaulimbiu isemayo “Madini ya Viwandani kwa Uchumi Wetu na Mazingira Bora”.
Amesema lengo kuu la mkutano huo ni kujua Kwa uhalisia kutoka kwa wahusika wa viwanda na wachimbaji ili kuwa Kwanini viwanda vya Tanzania vinatumia rasilimali za Tanzania.
Dkt.Mwasse amesema amesema kuwa katika mkutano huo wanaenda kukutanisha makundi matatu ambayo ni wenye viwanda,wachimbaji wadogo na wataalamu wa maabara.
“Kupitia mkutano huo wanatarajia kupata ufumbuzi wa changamoto mbalimbali zinazokabili sekta hiyo na jinsi ya kushirikiana na wenye viwanda ili kuuza malighafi zao na utengenezaji bidhaa zenye ubora,”amesema na kuongeza
“Mkutano huo ni jitihada za kumuunga mkono Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ili kuendana na mfumo uliojitokeza kuhusu ajenda ya viwanda ambapo madini yanayochombwa Tanzania yanaweza kupata soko,”amesema.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la wenye Viwanda Tanzania (CTI) Leodigar Tenga amesema idadi kubwa ya viwanda vikubwa hapa nchini vinategemea malighafi toka kwa wachimbaji madini kwa asilimia zaidi ya 80 hivyo mkutano huo ni fursa kubwa kwa wenye viwanda.
Hivyo amewataka wenye viwanda kushiriki kwa wingi katika mkutano huo ili kujadiliana na wachimbaji kuhusu upatikanaji wa malighafi bora za viwandani.
Kwa upande wake Katibu wa Chama cha Wanawake Wachimbaji Madini Tanzania (TAWOMA) ,Salma Ernest ameishukuru STAMICO kwa kuandaa mkutano huo ambao utasaidia kutambua fursa mbalimbali zilizopo kwenye sekta ya madini na viwanda.
More Stories
Wanafunzi 170 wapata ufadhili wa masomo
Maelfu kunufaika namsaada wa kisheria Katavi
Serikali yazidi kuwakosha wawekezaji wadau waipa tano