December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Dkt. Biteko mgeni rasmi mdahalo wa kumbukizi miaka 40 ya hayati Sokoine

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online

NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko leo tarehe 8 Aprili, 2024 anashiriki katika Mdahalo wa Kitaifa wa Kumbukizi ya Miaka 40 ya Hayati Edward Sokoine unaofanyika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kilichopo mkoani Morogoro.

Mada kuu katika mdahalo huo ni “Urithi wa Taifa na Uongozi wake, Bidii, Uadilifu na Uaminifu.”

Viongozi wa serikali na wadau mbalimbali wamehudhuria mdahalo huo.