Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Leo tarehe 16 Disemba 2023, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko anashiriki Mahafali ya 26 ya Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino cha Tanzania ( SAUT) yanayofanyika katika Viwanja vya Raila Odinga jijini Mwanza.
Mara baada ya kuwasili katika Mahafali hayo, Dkt. Biteko alipokewa na viongozi wa Chuo hicho wakiongozwa na Mkuu wa Chuo, Mhashamu Baba Askofu Mkuu, Gervas Nyaisonga ambaye ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mbeya na Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC).





More Stories
Kapinga :Zaidi ya nyumba 800 Mtwara kuunganishwa na mfumo wa gesi ya kupikia
Ilemela yatenga milioni 920 kwa ajili ya mikopo ya vikundi
Tabora Network yawezesha vijana kiuchumi