May 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Dkt. Biteko awasili Kenya kuhudhuria mkutano wa EAPP

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewasili nchini Kenya kuhudhuria Mkutano wa 18 wa Baraza la Mawaziri wanaohusika na mfumo wa pamoja wa umeme kwa nchi za Mashariki ya Afrika (EAPP Council of Ministers) utakaofanyika tarehe 27 na 28 Februari, 2024 jijini Nairobi.

Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA), Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati amepokelewa na viongozi mbalimbali wakiongozwa na Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Mhe. Benard Kibesse akiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati wa Kenya, Mhe. Alex Wachira pamoja na Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Stephen Byabato.