Na Judith Ferdinand, Times majira Online, Mwanza
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt.Angeline Mabula,ameeleza kuwa kupitia Katibu Mkuu wa Wizara hiyo ataunda tume itakayofanya uchunguzi kufuatia uwepo wa malalamiko juu ya vigogo kumilikishwa viwanja katika eneo la Isamilo lililopo Halmashauri ya Jiji la Mwanza.
Ambapo tangazo la serikali la uuzwaji wa maneo hayo lililotolewa mapema mwezi Juni mwaka huu na Halmashauri ya Jiji la Mwanza.
Dkt.Angeline ameyasema hayo katika mkutano na waandishi wa habari wa ufafanuzi juu ya utekelezaji wa vipaumbele vya bajeti ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa mwaka 2022/23,kilichofanyika jijini Mwanza Julai 13,2022.
Ambapo ameeleza kuwa katika suala la kuomba viwanja linakuwa wazi kwa mtu yoyote ata kama ni mtumishi wa Serikali hazuiliwi kuomba kiwanja ili mradi amefuata utaratibu kama wengine.
“Kilio cha Mwanza tumekisikia ya kwamba wakilalamikia viwanja vya Isamilo kwamba wamepewa vigogo watupu,kama Wizara nimeisha muelekeza Katibu Mkuu aweze kuunda tune ije kufanya uchunguzi, ili kuona ni halali au malalamiko hayo ni ya kweli,”ameeleza Dkt.Angeline na kuongeza kuwa
“Kama waliomba kwa utaratibu ambao wameomba wengine hapata kuwa na kesi kama wamezunguka nyuma ya mlango kama wanavyosema basi litakuwa ni jukumu jingine,naomba nisitoe maelekezo maana niliisha toa maelekezo baada ya kuona kilio hicho kwenye magazeti na luninga,”.
Pia ameeleza kuwa,jumla ya hati miliki milioni 2.4 zimeisha andaliwa mpaka Sasa na Wizara hiyo umilikishaji wa hati changamoto wananchi hawalipi kama inavyotakiwa.
“Kuna wananchi wakipimiwa maeneo anatambua kiwanja chake na plot namba yake lakini haji kuomba umiliki na hapa Mwanza tunayo mifano mingi tu,ambapo kitaifa tuna zaidi 900,000 ambao wameisha pimiwa na kila kitu kimekamilika anatakiwa kulipa pesa kwa ajili ya kumiliki halipi,”ameeleza.
“Mwaka jana au juzi tulipitisha sheria ya kuwa mtu unakiwanja chako na kimekamilika kupimwa unaanza kulipia kodi na haijalishi kina hati au hakina hati,hiyo yote ni kutaka kuona watu wanaomba kumilikishwa,”.
Aidha ameeleza kuwa Wana hati zaidi ya 24,000 nchi nzima kwa ofisi za wasajili ambazo zinekamilika lakini watu hawajaenda kuchukua hati zao huku akihoji kuwa sijui watu bado hawajajua umuhimu wa hati na kuwa zinaweza kuwasaidia kunufaika kiuchumi.
Kwa wakati huo huo Dkt.Angeline ameeleza kuwa suala la fidia, migogoro mingi ya ardhi iliopo ni katika zile kesi za miaka nenda rudi ambapo mwaka 2016 walipitisha sheria namba 7 ya uthamini ikimruhusu mtu akichukua eneo la mtu baada ya miaka miwili kuwa ameisha lipa fidia.
Endapo katika muda huo kama fidia haijalipwa mwenye eneo yupo huru kuendelea na kazi zake na yule mtu kama analitaka eneo tena itabidi afanye uthamini upya kwa sababu ule uthamini wa mwanzo utakuwa umepitwa na wakati.
“Sheria na kanuni zake za mwaka 2018 zimeweka bayana lakini kama Wizara tumeisha zungumzia kwa msisitizo sheria hii baada ya kuona uthamini wa viwanja vingi ambavyo fidia haijalipwa tumesema hakuna eneo la mtu linaloweza kuchukuliwa bila kulipwa fidia,ili kuondoka na madai yaliopo na kumchelewesha mwananchi kufanya shughuli zake ukitaka eneo la mtu njoo na pesa taslimu,”ameeleza Dkt.Angeline.
Sanjari na hayo Waziri huyo amewataka wananchi kushiriki kikamilifu katika zoezi la urasimishaji wa makazi.
“Ni kweli zoezi la urasimishaji wa makazi kwa mujibu wa mpango lilianza mwaka 2015 na linatarajiwa kukamilika mwaka 2023,kwani kumekuwa na changamoto ya kubwa ya wananchi kutoshiriki katika zoezi hilo ili maeneo yao yaweze kutambuliwa,”.
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa