January 8, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Dkt.Angeline aelezea fursa za kiuchumi stendi ya mabasi na maegesho ya malori Nyamhongolo

Na Judith Ferdinand, TimesMajira Online, Mwanza

Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mbunge wa Jimbo la Ilemela Dkt.Angeline Mabula ameeleza kuwa mradi wa stendi ya mabasi na maegesho ya malori Nyamhongolo wilayani Ilemela,utawanufaisha wananchi wa Ilemela,Mkoa na jamii kwa ujumla.

Ambapo ameeleza kuwa kuna fursa mbalimbali zitakazowawezesha wanaIlemela na jamii kwa ujumla kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi ambazo zitawanufaisha wao na taifa kwa ujumla.

Akizungumza kwa njia ya simu na majira/Timesmajira online Dkt.Angeline amesema,katika kipindi hiki ambacho Rais Samia ameingia madarakani ameendelea kufadhili mradi huo ambao umeendelea mpaka umekamilika.

Dkt.Angeline amesema,anachoweza kuwaambia wananchi wa Ilemela kuwa mradi ule ni wa kimkakati ambao utanufaisha wanaIlemela,watu wa Mwanza lakini na jamii kwa ujumla kwa sababu mabasi yatakayokuwa yanaingia na kutoka ndani ya stendi hiyo yatakuwa yanatoka mikoa mbalimbali.

Hivyo wananchi watakuwa wanufaika katika kufanya biashara na mambo mengine lakini pia kuna malori ambayo yatakuwa yanaleta mizigo.

Amesema ni stendi ya aina yake kwa sababu siyo stendi zote nchini zilizo jengwa zimeunganishwa na huduma hiyo ya malori lakini kuna huduma ya hosteli ambayo iko pale ambapo kwa wale wasio taka usumbufu wanaweza kulala na kuamka pale kisha kuendelea na safari.

Pia amesema,zamani watu walikuwa wanapata shida katika suala la usafiri sababu stendi ipo mbali Nyegezi na pengine mfano mtu anakaa Igombe,lazima aamke alfajili au aende alele kule kwaio kulikuwa na gharama kubwa za watu kuweza kupata usafiri maeneo ya mbali ila kwa sasa usafiri upo karibu.

“Naishukuru sana serikali kwa sababu miradi ya kimkakati imepewa kipaumbele katika maeneo mengi,
mradi ulianza kwa kusuasua sana siku za mwanzo kidogo tungeweza kuukosa huo mradi lakini nilijitahidi kama muwakilishi kuweza kuwasemea wananchi na kuona hali halisi itakayoweza kubadilisha maisha yao kama mradi huo utakubalika na serikali ilinisikiliza na mradi huo ukaendelea mpaka umekamilika” amesema Dkt.Angeline.

Lakini pia Dkt.Angeline amesema mradi huo umesheheni huduma mbalimbali ikiwemo za benki ambapo wametenga maeneo kama matatu kwa ajili ya benki,mini super market,migahawa ndani ya eneo kama mtu anataka huduma mbalimbali za kijamii pale anazipata.

Wameweka maduka mengi karibu 74 ambayo sasa wenye maduka wanaweza kufanya biashara zao pale abiria anayeshuka anaweza kununua kitu na kwenda nacho kama zawadi huku wenye mabasi wametengewa ofisi zao kwa ajili ya huduma hiyo hivyo huduma ambayo inayotakiwa kuwepo kwenye stendi ya mabasi imekuwepo pale.

Sanjari na hayo Dkt.Angeline amezungumzia fursa ya machinga katika kufanya biashara katika eneo hilo ambapo amesema Wana mpango wa kujenga jengo kwa ajili ya machinga kufanya shughuli zao.

Amesema,machinga nao watakuwa na jengo lao pembeni ya stendi,mradi huo umekwisha,sasa wanategemea kuanza mradi mwingine wa machinga jirani na stendi ambapo hasa wateja wao ndioo walipo anapotaka kusafiri anaweza kupita kwa machinga pale akanunua kitu akaendelea na safari.

“Tunajua maeneo kama hayo bado machinga wanahitaji kufanya biashara zao,kwa sababu ni stendi ya kisasa tusinge penda kuwa na mchanganyiko huo,tunachosubili sasa hivi baada ya ufunguzi na kwa mpango tulionao kama wanaIlemela kwa pembeni yake kuna kiwanja ambacho kitajengwa machinga complex,” amesema Dkt.Angeline.

Hivyo ametoa wito kwa wananchi kutunza miundombinu ya mradi huo kama ambavyo wameipokea jinsi ilivyo,hawaitaji kufanya uharibifu wowote kizazi kijacho hakitakuta kitu.

“Tushukuru Mungu kwamba mradi umekwisha udokozi ulikuwepo mwanzoni ambao ulidhibitiwa na watu wakatambua kwa sababu mimi nilitembelea huu mradi zaidi ya mara nne nikawa nazungumza na wahusika,nikazungumza na vibarua nikawaambia msifanye vitendo vyovyote vya kuhujumu mradi maana unakuwa unajihujumu mwenyewe nashukuru kwamba waliweza kufanya vizuri zaidi hawakuweza kuendelea na udokozi na kazi imefanyika vizuri,” amesema Dkt. Angeline na kuongeza kuwa

“Ukisikia historia ya mradi huu serikali ya awamu ya sita imeweza kuwatendea haki wanaIlemela,Rais Samia ni mlezi wa Ilemela wa hiari alijitolea mwenyewe, tunamshukuru mlezi wa Ilemela,Rais wetu kwa kuhakikisha mradi wetu umekamilika na unaanza kazi na kuwanufaisha Watanzania na uchumi unakwenda kupaa,”.

Hata hivyo Machi 9 mwaka huu,Mkandarasi Mshauri Mkuu wa mradi wa ujenzi wa kituo cha mabasi na malori Nyamhongolo kutoka chuo Kikuu cha Dar es Salaam kupitia BICO,alikabidhi mradi huo kwa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela chini ya usimamizi wa Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel.

Ambapo ujenzi wa mradi huo hadi kukamilika kwake umegharimu kiasi cha bilioni 26.6.